Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Mwanamvua Mrindoko( katikati) akiwa na baadhi ya viongozi wa mkoa na kitaifa wa CWT.
Na Walter Mguluchuma KTPC,Katavi .
Chama cha Walimu Tanzania (CWT( kimeiomba Serikali kutowaweke muda mrefu walimu wanaofundisha Shule za Msingi na Sekondari kwenye maeneo ya Makazi ya Wakimbizi ili wasizeekee huko bila kujiandalia mambo mengine ya kimaisha kama vile kujenga makazi ya kudumu .
Ombi hilo ametowa wakati wa mkutano mkuu wa sita wa umoja wa ujirani mwema Nyanda za juu kusini( SOHITCO( uliofanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi ambao umewashirikisha viongozi wa cwt wa kutoka katika Mikoa sita ya Katavi , Rukwa, Songwe, Mbeya, Njombe na Iringa .
Akisoma Risala ya wasshiriki wa mkutano huo mbele ya mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko katibu wa CWT Mkoa w Katavi Nuru Shenkalwa alisema kumekuwa na changamoto kwa walimu wanaokuwa wamepangiwa kufanya kazi kwenye vituo vya makazi ya wakimbizi kuweza kujenga makazi yao ya kudumu kutokana na sheria zinazo kataza watu kujenga nyumba za kudumu katika makazi ya wakimbizi yaliko katika Mkoa wa Katavi .
Hivyo wanaiomba Serikali Walimu walioko kwenye Shule hizo watazmwe ili ili wasikae muda mrefu ili wasije wakazeekea huko bila kujiandalia mambo yao mengine ya kimaisha mfamo kujenga makazi
yao ya kudumu .
Aidha alisema kuwa watakuwa wachoyo wa fadhila kama hawataishukuru Serikali kwa kupandisha vyeo vya walimu katika maeneo yao hali hiyo imeondoa manung-ununiko ya muda mrefu na kuwarudishia matumaini mapya .
Mweka Hazina Hazina wa CWT Taifa Aboubakar Allawi alieleza kuwa chama hicho kinaishukuru Serikali kwa hali ambayo inayoendelea sasa ya kuboresha miundo mbinu ya kufanyi kazi walimu pamoja na makazi yao ya kuishi . PAMOJA
Alisema kuwa anapenda kuikumbusha Serikali kushughulikia swala la walimu 66,000 ambao majina yao yalihakikiwa mwaka 2017 kwa ajiri ya kupandishwa madaraja lakini hadi sasa swala lao halijashughulikiwa hari ambayo imekuwa ikileta malalamiko ya walimu kwenye chama chao kuanzia kwenye matawi hadi Taifa .
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko alibainisha kuwa Serikali itaendelea kutowa ushirikiano kwa chama cha Walimu Tanzania na vyama vingine vya wafanyakazi ili viweze kutimiza majukumu yao vizuri .
Alifafanua kuwa hakuna sehemu ambapo maendeleo yameonekana au kufanyika bila kutaja jina La mwalimu katika kuchangia maendeleo hayo hivyo watambue kuwa wao ni watu muhimu sana na Serikali inawategemea .
Alisema Serikali imejipanga kuhakikisha walimu wote wanaishi kwene mazingira mazuri na bora kwani inatambua kuwa bado kuna baadhi ya maeneo wanayoishi sio bora.