Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi,Benjamin Kuzaga.
Na Mwandishi Wetu KTPC,Katavi.
Ujenzi wa bandari ya Karema ya kimkakati inayoendelea kujengwa katika wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi itakayotumika kwa ajili ya kusafirishia mizingo na abilia kutoka Tanzania kwenda nchi ya DRC Congo baada ya kukamilika,Ujenzi huo umeanza kuhujumiwa kwa kufanyika wizi wa vifaa mbalimbali.Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Mwanamvua Mrindoko.
Uhujumi huo umebainika baada ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi kufanya operesheni ya misako na doria maalumu ya kudhibiti mtandao wa wizi wa rasilimali za mradi wa ujenzi wa bandari ya Kimkakati ya Karema na kufanikiwa kukamata watuhumiwa 16 wakiwa wameiba mafuta ya diseli lita 4,100 na nondo 68 na vifaa mbalimbali mali ya kampuni inayojenga bandari hiyo.
Kamanda wa Jeshi la Polisi wa Mkoa wa Katavi,Benjamin Kuzaga amewaambia wandishi wa habari kuwa watuhumiwa hao walikamatwa huko katika Vijiji vya Karema na Ikola kufuatia msako makali ulifanywa na jeshi hilo.
Amesema kuwa kabla ya kufanyika kwa msako huu mkali jeshi Polisi walipata taarifa juu ya hujuma zinazofanywa za wizi kwenye ujenzi huo wa bandari ya Karema inayotarajiwa kukamika kwa ujenzi wake hapo 6 March 2022.
Baada ya taalifa hizo kufika kwa jeshi la polisi walifanya msako mkali na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa 16 wakiwa na mafuta aina ya diseli lita 4,100, vipande 58 vya nondo , madumu 118 ya plasitiki ,betri mbili za gari grisi kilo saba na oili lita 10 vyote vikiwa mali ya Kampuni ya XIAMEN ON COING CONSTRACTION GROUP COMPANY LIMETED inayotekeleza mradi wa kimkakati wa ujenzi wa bandari y a Karema.
Baadhi ya maduma ya mafuta ya dizeli yaliyoibiwa.
Kamanda Kuzaga amewataja watuhumiwa hao waliokamatwa kuwa ni Jackson Mathias Mkazi wa Ikola ,Godfey Kigongo ,Joseph Haule wakazi wa Kijiji cha Karema , Ibrahimu Simba Mkazi wa Kijiji cha Inyonga , Ayubu Athuman, Chuki Wiliam,,Jipala Nekala , Lusonguye Kaise , Jacob Thobias Muse Enelil Benedictor w ote wakazi wa Karema .
Ameeleza kuwa watuhumiwa wote wanaendelea kuhojiwa kuhusiana na matukio hayo ya wizi na mara baada ya taratibu zote za kiupelelezi kukamilika jalada litafikishwa katika ofisi ya Taifa ya mashitaka Mkoa wa Katavi kwa hatua zaidi za kisheria.
Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Mwanamvua Mrindoko akizungumza na wananchi.
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko amewaagiza watu wote ambao wamehusika na wizi kwenye mradi huo wajisalimishe kabla hawaja kamatwa kwani endapo kama watashindwa kusalimisha mali walioiba wakikamatwa watachukuliwa hatua kali ikiwemo kuwekwa mahabusu bila kutoka kwani kosa hilo lina husiana na kuhujumu uchumi.
Amesema kuwa kitendo hicho cha wizi ni aibu kwani mradi huu umewekwa kwa ajiri ya kuwasaidia badala yake wao ndio wamekuwa watu wanaofanya uhalifu ni aibu na wala Serikali ya Mkoa haita wavumilia hata kidogo.