Mkuu wa Mkoa wa Katavi Bi.Mwanamvua Mrindoko
Na Paschal Katona
Katavi
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko amekabidhiwa vyumba vya madarasa 59 vilivyogharimu shilingi Bilioni 4.2 na kuagiza wazazi na walezi kuhakikisha ifikapo Januari 17, 2022 wanafunzi wote wanaotakiwa kuwa shule waripoti kuanza masomo.
Mrindoko ameonya pia mzazi au mlezi atakayeshindwa kumpeleka mtoto wake shule hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
Kauli hiyo ameitoa wakati anakabidhiwa vyumba vya madarasa 59 katika Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi na kuweka jiwe la Msingi katika shule ya Sekondari Shanwe
Akisoma risala kwa Mgeni mualikwa Mkuu wa Idara ya Mipango Manispaa ya Mpanda Waza Benjamin ameeleza kuwa majengo hayo 59 yamekamilika kwa asilimia mia moja.
Kamishna msaidizi wa jeshi la zimamoto na uokoaji Regina Kaombwe ambaye ni Mwenyekiti wa kamati ya ujenzi Manispaa ya Mpanda ameelezea kuridhishwa na ujenzi huo na kuwa hakuna udanganyifu wowote uliofanyika katika ujenzi wa vyumba hivyo vya madarasa.