MWANAMKE AKAMATWA NA DAWA ZA KULEVYA,BANGI KETE 432 MKOA WA KATAVI

 


Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi,ACP Ali Makame Hamad

Na Walter Mguluchuma

     Katavi

Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi limefanikiwa kukamata madawa ya kulevya aina ya bangi,pombe ya moshi pamoja na silaha aina ya gobore katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi,ACP Ali Makame Hamad akitoa taarifa kwa vyombo vya habari alisema kuwa kuelekea sikukuu za Xmas na Mwaka Mpya wamefanikiwa kumkamata Anastazia Joseph (47) mkazi wa Society akiwa na madawa ya kulevya aina ya  bangi kiasi cha kete 432 na gramu 1,250 za madawa ya kulevya.

Hamad alieleza kuwa madawa hayo ya kulevya wameyakamata katika kata ya Magamba Tarafa ya Misunkumilo Wilaya ya Mpanda mkoa wa Katavi ambapo pia kwa kipindi cha wiki moja kuanzia Desemba,18 hadi Desemba 24 mwaka huu Jeshi hilo linawashikilia watuhumiwa 13 baada ya kukamatwa na jumla ya lita 317 za pombe haramu ya moshi.

Vilevile Jeshi hilo linamshikilia William Chacha(20) mkazi wa Kitunda akiwa na silaha aina ya gobore aliyoisalimisha  katika ofisi ya Mtendaji wa kijiji cha Wachawaseme kata ya Utende,Tarafa ya Inyonga Wilaya ya Mlele.

Na watuhumiwa wote mara baada ya upelelezi kukamilika wamefikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakanili.

Katika hatua nyingine Jeshi la Polisi limewatahadharisha wananchi wa Mkoa wa Katavi kwa kipindi hiki cha sikukuu za Xmas na Mwaka Mpya  kuwa wanachukua  tahadhari za kukabiliana na changamoto mbalimbali za matukio ya kihalifu yanayoweza kuzorotesha ulizi na usalama wa raia na mali zao.

Katika kuhakikisha matukio kama hayo hayajitokezi na kuleta athari wananchi wanatakiwa kuepukana na mazingira hatarishi wakati wa sikukuu kwa kutosherehekea mbali na makazi yao.

Kwa watumia vileo,kutolewa kupita kiasi cha kushindwa kufanya maamuzi sahihi,Madereva na wamiliki wa vyombo vya moto kufanyia matengenezo vyombo vyao ikiwa ni pamoja na kuzingatia sheria za usalama barabarani na kutowaacha watoto wadogo kuzurura hovyo pasipo uangalizi ilikuepukana na ajali za barabarani za kufa maji au kupotea.

Tahadhari nyingine ambazo wananchi wamepewa ni pamoja na kuimarisha ulinzi kwenye makazi yao kwa kuwaacha walinzi/waangalizi wa kulinda usalama wa mali zao pamoja na majirani zao.

Kamanda alisisitiza kwa watakao kwenda kwenye kumbi za starehe wajiepushe na misongamano isiyo ya lazima kwani yaweza kuleta madhara kiafya na pengine ushawishi wa kihalifu kama wizi na uporaji.

Aidha kwa wamiliki wa kumbi za starehe wametakiwa kuhakikisha wanaandaa mazingira rafiki na salama kwa wateja wao na wamiliki wa nyumba za kulala wageni wanatakiwa kuzingatia sheria na taratibu za kupokea wageni kwa kuwahoji na kutoa taarifa zao.


Jeshi la polisi Mkoa wa Katavi  limejipanga kuhakikisha linadumisha hali ya ulinzi na usalama kwa kufanya doria za kutambulika na kutotambulika usiku na mchana maeneo yote pamoja kuhakikisha hatua kali za kisheria zinachukuliwa kwa mtu au kikundi chochote kitakacho bainika.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages