WAANDISHI WA HABARI WAHIMIZWA KUPAZA SAUTI KWA WANANCHI JUU YA UTUNZAJI WA MAZINGIRA

 

Waandishi wa Mikoa ya Rukwa,Katavi,Tabora na Kigoma  katika picha ya pamoja baada ya Kupatiwa Mafunzo ya Utunzaji wa Mazingira yaliyofanyika Mkoa wa Kigoma


Na Walter Mguluchuma

Kigoma

Vyanzo vya maji kuvamiwa na shughuli za kibinadamu ikiwemo kilimo na ufugaji kumesababisha kupungua na kuharibika kwa vyanzo hivyo hali inayopelekea kukosekana kwa maji na elimu kuhitajika kwa jamii. 

Waandishi wa Habari wa Mikoa ya Kanda ya Magharibi wamehimizwa kupaza sauti za kuelimisha jamii kwa ajili ya utunzaji wa mazingira ili wananchi waone umuhimu wa kutunza mazingira .

Wito huu umetolewa na Mratibu wa kuwajengea uwezo Waandishi wa Habari za Mazingira wa Mikoa ya Katavi Tabora , Kigoma na Rukwa Prospe Kwigize katika mafunzo yaliyoandaliwa na GOOD HARVEST ORGANISATION kwa kushirikiana na Buha Radio Fm Mkoa wa Kigoma .

Kwigize amebainisha kuwa kutokana na umuhimu wa utunzaji wa mazingira na mabadiliko ya tabia nchi wameamua kutowa mafunzo kwa Wandishi wa Mikoa hiyo ili waweze kubobea katika uandishi wa habari za uhifadhi wa Mazingira.

Hivyo amewahimiza Waandishi wa Habari kupaza sauti ili wananchi waweze kuona umuhimu wa kutunza mazingira yasiendelee kuharibika yawe na manufaa katika kizazi cha sasa na kijacho .

Kwigize ameeleza kuwa mafunzo hayo yatawajengea Waandishi wa Habari uwezo wa namna ya kushiriki kuandika habari za mazingira kwenye jamii na hali ya mabadiliko ya tabia nchi .

"Matarajio ya mradi ni kuwa na Waandishi wa Habari mahiri katika kuandika habari za mazingira pia mradi unatarajia kufika katika Mikoa ya Songwe na Mbeya"alisema Kwigize

Water Resources Engineer and head of environmental and projection department wa Bonde la Ziwa Tanganyika Eng Odemba Kornel alieleza baadhi ya changamoto ambazo zimekuwa zikisababisha kuwepo kwa uharibifu wa mazingira na vyanzo vya maji kwenye mikoa ya Rukwa,Katavi,Tabora na Kigoma.

Vyanzo vingi vya maji kuingiliwa na shughuli za kibinadamu kama vile kilimo na ufugaji na kusababisha vyanzo vya maji kupungua na kuharibika.

Hivyo wao kama wasimamizi wa bonde moja ya majukumu yao ni kuhakikisha kuwa lazima maji yatumike vizuri kama zinavyotumika vizuri rasilimali nyingine za nchi ndio maana Serikali imeweka kipaumbele kuhakikisha vyanzo vya maji vinakuwa salama .

Amesisitiza kuwa bonde wanahakikisha vyanzo vya maji vyote vinatunzwa kwa kuzingatia sheria za nchi zinazohusiana na mazingira na mabonde pamoja na vyanzo vya maji .

Nae Mhandisi wa Rasilimali za Maji wa Ziwa Tanganyika Gaudens John Ndolo ameeleza matokeo yameanza kuonekana kwa baadhi ya maeneo watu wameacha kulima kwenye vyanzo vya maji .

 "Matokeo hayo yametokana na elimu ambayo tumekuwa tukiitowa kwa wananchi juu ya uhifadhi wa mazingira na jitihada hizo za elimu zikiendelea kutolewa pia na Waandishi wa Habari itasaidia kumaliza uharibifu wa mazingira"



Waandishi wa Habari za Mazingira kutoka Mkoa wa Rukwa,Katavi,Tabora na Kigoma wakifuatilia kwa umakini Mafunzo ya Utunzaji wa vyanzo vya Maji.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages