UJUZI WA ELIMU YA KIDIGITALI FURSA KWA WAANDISHI WA HABARI.

 



Na Irene Temu

Katavi

Ujuzi wa Elimu ya Kidigitali kwa Waandishi katika vyombo mbalimbali vya Habari vilivyopo hapa nchini imekuwa fursa kufanya mageuzi ya uandishi wa Habari kimtandao na kuupa uandishi thamani.

Vyombo vya Habari hapa nchini vimetakiwa kuendana na Kasi ya Sasa ya upashaji wa Habari kwa kutumia ujuzi wa Kidigitali ili kuendana na Kasi ya dunia na ulimwengu kwa ujumla inayotumia Elimu ya Kidigitali kupasha jamii Habari mtandaoni.

Women At Web Tanzania kwa kushirikiana na Media Convergency wanatoa Mafunzo ya Elimu ya kidigitali kwa Waandishi wa Habari hapa nchini lengo likiwa ni kuwapa ujuzi wa kutumia fursa zinazopatikana mtandaoni na kutumia fursa kuupa uandishi thamani.

Zahara Tunda ni miongoni mwa watumiaji wa mtandao katika utendaji kazi wake aliwataka Waandishi kufahamu umuhimu wa kutumia mitandao katika kazi za uandishi na manufaa wanayoweza kupata kwa kutumia mitandao hiyo kuandika na kuchapisha Habari zao pia kuweka mawasiliano mtandaoni.

Mwandishi wa Habari Haruna Juma anasema matumizi ya kidigitali hutoa fursa ambazo zinaweza kusaidia msingi wa kifedha wa vyombo vya habari ikisimamiwa vyema.

Pia anaeleza matumizi ya Elimu ya kidigitali katika mitandao inaweza kutengeneza mapato ya ziada, wateja zaidi na njia mpya za usambazaji wa habari ambazo zinaweza kuchangia katika kuongeza uhuru wa vyombo vya habari.

"Baadhi ya viongozi wa vyombo vya habari nchini tayari wameachwa nyuma na teknolojia ya matumizi ya elimu ya kidigitali huku wakikabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo ukosefu wa mtandao wa intaneti ya uhakika,vifaa dhaifu vya teknolojia na ustadi wa chini wa wafanyakazi katika vyombo hivyo juu ya matumizi ya kidigitali"anaeleza Mwanahabari Haruna 

Anasema haya yote yanatokea wakati sehemu nyingine za dunia zinasonga mbele kwa kasi kubwa na hali ya kidijitali inayobadilika kila leo.

Nae Mwandishi wa Habari gazeti la Nipashe Neema Hussein anasema kuwa baadhi ya nchi ulimwenguni kutangulia kutumia elimu ya kidigitali Kuna faida kwani viongozi wa vyombo vya habari hapa nchini wanaweza kupata fursa ya kujifunza kutokana na makosa ya wengine na hivyo kuepuka kujirudia kwao wakati wakitumia elimu ya kidigitali kuchapisha Habari Kimtandao.

Pia wanaweza kujaribu na kutumia baadhi ya njia za Kimtandao ambazo tayari zinafanya kazi katika sehemu nyingine za dunia na kuziendeleza zaidi baada ya kupata elimu ya kidigitali.

Hata hivyo wanaweza kulinganisha mbinu muhimu ambazo vyombo vingine vya habari vya Kiafrika vilivyofanikiwa tayari vimepitia na kuzianzisha baada ya kupata elimu ya Kimtandao na kuanza kutumia.

Elimu ya kidigitali na matumizi yake katika jamii imeonekana kushika Kasi huku Waandishi wa Habari wengi wakichukua maamuzi ya kufanya kazi kimtandaoni zaidi baada ya kupata elimu na kujua umuhimu wa kutumia mitandao katika kazi ya Uandishi.




Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages