UZINDUZI WA UGAWAJI WA VYANDARUA BURE KWA WANANCHI WA MKOA WA KATAVI WAZINDULIWA


Mratibu wa malaria Mko wa Katavi Dr Ramadhani Karume

Na Mwandishi wetu

Katavi

Serikali ya Mkoa wa Katavi kwa kushirikia na Wizara ya Afya,Maendeeo ya Jamii Jinsia,wazee na watoto imehakikishia jamii ya wanakatavi ifikapo mwaka 2030 watakuwa wametokomeza ugonjwa wa malaria ambao umeonekana kuwa tatizo linalosababisha vifo vingi kwa watoto wa umri chini ya miaka mitano na Wajawazito katika Mkoa wa Katavi na Taifa kwa ujumla ambapo maambukizi ya ugonjwa wa malaria kwa sasa ni asilimia 7 katika Mkoa wa Katavi.

Akiongea katika uzinduzi wa ugawaji vyandarua bure kwa kila kaya zilizopo ndani ya Mkoa wa Katavi,Mratibu wa Malaria Mkoa wa Katavi Dr Ramadhani Karume alisema mwaka 2030 wanatazamia kuwa ugonjwa wa malaria ndani ya Mkoa wa Katavi utakuwa umetokomea au kuisha kabisa na kuiacha jamii ya wanakatavi salama.

Dr Karume alisema bado maambukizi ya ugonjwa wa malaria unawakabili watoto waliopo chini ya umri wa miaka mitano na wajawazito hivyo serikali kwa kutambua hilo wameamua kugawa vyandarua bure kwa kila kaya ilikupunguza ukali wa ugonjwa huo kwa jamii na kunusuru uhai wa watoto wa chini ya umri wa miaka mitano na mama wajawazito.

Aidha alisema ugawaji wa vyandarua hiyo umezingatia idadi halisi ya wanafamilia waliopo katika kila kaya na kila mtu atagawiwa huku akisisitiza vyandarua hivyo vinagawiwa bure na serikali imevigharamia.


Mkuu wa Mkoa wa Katavi Bi Mwanamvua Mrindoko akizindua zoezi la utoaji wa vyandarua bure kwa wananchi wa Mkoa wa Katavi

Nae Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko aliwaasa wakazi wa Mkoa wa Katavi kutumia vyandarua hivyo kwa ajili ya kujikinga na ugonjwa wa malaria na sio kwenda kufugia kuku,kuzungusha katika bustani za mboga mboga au kuhifadhi kabatini hayo sio matumizi sahihi.

Mrindoko alisisitiza vyandarua hivyo vitumike kupunguza ugonjwa wa malaria ndani ya Mkoa wa Katavi na watendaji wote watakao tekeleza ugawaji wa vyandarua hivyo waifanye kazi hiyo kwa uaminifu na yoyote atakaye kwenda kinyume kwa kufanya ubadhilifu hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

“ugawaji wa vyandarua hivi nasisitiza uzingatie idadi ya wanafamilia katika kila kaya asiwepo mtua atakaye pewa chandarua pungufu na idadi ya watu waliopo katika familia yake au zaidi ya idadi iliyoandikwa katika kiambata chake alichokabidhiwa wakati wa uandikishaji wa idadi ya wanafamilia ili kufanikisha ugawaji wa vyandarua hivyo”alisisitiza Mrindoko.  


Mkazi wa Mkoa wa Katavi Spensioza Odas akikabidhiwa  chandarua bure na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko wakati wa uzinduzi wa zoezi la utoaji wa vyandarua vinavyotolewa na Wizara ya Afya

Nao baadhi ya wananchi waliopata fursa ya kugawiwa vyandarua katika zoezi hilo la uzinduzi lililoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko akiwemo Spensioza Odas ameipongeza serikali kwa kuwagawia chandua kwani imeonyesha kuwajali wananchi wake pamoja na afya zao.

Nae Mzee maarufu katika Mkoa wa Katavi Vicent Nkana ameushukuru uongozi wa serikali ya Mkoa wa Katavi kwa kuweka utaratibu mzuri wa kugawa vyandarua hivyo ambapo kila familia itapata chandarua na kujikinga na malaria na afya za wanakatavi zitaendelea kuwa imara na kufanya kazi kwa bidii wakiwa na afya njema.

  

 

 

 

 

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages