WAANDISHI WA HABARI WA KANDA YA MAGHARIBI WAPIGWA MSASA ELIMU YA UTUNZAJI WA MAZINGIRA .


 
Wandishi wa  Mikoa ya Kanda ya Magharibi walioshiriki Mafunzo ya Utunzaji wa Mazingira yaliyofanyika Ukumbi wa Katavi Resort Mkoani Katavi

 Na Walter Mguluchuma

KATAVI.

Waandishi wa Habari wametakiwa  kujikita kuandika habari za mazingira kwani wanakosa  fursa  za  kuandika  habari zinazohusu mazingia  na matokeo yake  wamekuwa  hawaleti tija kwenye jamii na masuluhisho yanayo ikabili juu ya mabadiliko ya Tabia nchi.

  Wito huu umetolewa na Prosper Kwigize mwezeshaji wa mafunzo   kwa waandishi wa Mikoa ya Katavi , Tabora , Kigoma na Rukwa yaliyohusu utunzaji wa mazingira yaliyofanyika katika Ukumbi wa Katavi Resort Mkoani Katavi yaliyoandaliwa na Taasisi ya Uhifadhi wa Mazingira ya Good Harvest Organization kwa Kushirikiana na Buha Fm Radio The Voice of Kigoma.

Kwigize amebainisha kuwa vyuo vingi vya Uandishi wa habari hapa Tanzania havifundishi Uandishi wa Ubobezi wa vitu kama Mazingira,Afya, na Biashara matokeo yake tunakosa fursa za kuandika habari kwa Tija tofauti na waandishi wa nchi za ulaya ambao wao hubobea kusomea uandishi wa jambo moja na sio kuandika kila kitu.

Alisema kwa kutambua hilo  Taasisi  ya Good Harvest Organization na Buha Radio fm wameona umuhimu kuwapatia Mafunzo maalumu waandishi wa Habari wa Mikoa ya Magharibi ya kuwajengea uwezo wa kuandika habari zinazohusu mazingira kwa ufasaha.

Kwigize alisisitiza kila Mwandishi alieshiriki Mafunzo hayo kuandika habari ambazo kesho yake zitatoa matokeo chanya kwa wananchi kutochoma misitu Moto na habari hiyo itakuwaimeleta mchango wa kuthibiti athari za mabadiliko ya tabia nchi.

 "Mfumo wa Uandishi wa Habari za kitanzania mara nyingi sioshirikishi kwa watu wa kawaida ni mfumo ambao waandishi wanaandika zaidi habari za viongozi kwa asilimia sabini au sitini wananchi wao wanapewa nafasi kidogo ya asilimia kumi na ishirini wakati wao ndio wanaoumia na kufanya uharibifu wa mazingira  hivyo waandishi acheni kuwa vipaza sauti za viongozi na badala yake tuwe vipasa sauti za wananchi kwa kuwashirikisha kwa yale tunayo andika sisi waandishi"Alifafanua Kwigize

Nae Rais wa Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa Habari Tanzania (UPTC) Deogratias Nsokolo alisema ukanda wa Mikoa ya Magharibi ukilinganisha na Kanda nyingine inaonekana ipo salama lakini sisi tunaoishi huku tunaona hatupo salama sababu jirani akihalibikiwa anaefata ni wewe .

Kwahiyo waandishi waliopata mafunzo haya wameanza safari ya kuelimisha jamii juu ya kurejesha uoto wa asili kwa kushirikiana na wadua mbalimba wa uhifadhi wa mazingira.

Kwa upande wake Silesi Malli Malli ambae ni Mwenyekiti wa Muungano wa Jumuiya za Umoja wa Mataifa Tanzania yaani[ United Nations Association of Tanzani[UNATZ] amesema wanawake wamekuwa ni nguzo kubwa katika uendeshaji wa familia zao na wengi wanategemea ujasiliamali ukiwemo upishi lakini kama kuna mabadiliko ya tabia nchi wa kwanza anaeathirika ni Mwanamke .

Amewahimiza wanawake kushiriki kikamilifu katika shughuli za kukabiliana na Mabadiliko ya Tabia nchi ikiwemo Upandaji wa miti,Kutunza mazingira na kuto lima katika vyanzo vya maji kwasababu wao ndio waathirika wakubwa wa mabadiliko ya Tabia nchi hivyo lazima washiliki katika mapambano hayo kwa vitendo.


Rais wa Vilabu vya Waandishi wa Habari Nchini  Deogratius Nsokolo katikati akiwa na Mwenyekiti wa Chama cha  Waandishi wa Habari Mkoa wa Katavi  Walter Mguluchuma kushoto  pamoja  na Mwandishi wa Azam TV Mkoa wa Tabora Juma Kapipi.


Mkurugenzi wa Good Harvest Organization Filbert Chundu akiwa katika picha na Mkurugenzi wa Buha FM Prosper Kwigize ambae alikuwa Mkufunzi wa mafunzo hayo.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages