NAIBU WAZIRI WA AFYA DR GODWIN MOLLEL AHIMIZA HOSPITALI YA RUFAA MKOA WA KATAVI KUKAMILIKA KWA WAKATI


Naibu Waziri wa Afya Dr Godwin Mollel (wa pili kushoto)akiwa katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Katavi inayoendelea kujengwa


Na Irene
 Temu

Katavi

Naibu Waziri wa Afya Dr.Godwin Mollel amewataka wasimamizi wa mradi wa Ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi unaoendelea kuhakikisha Ujenzi huo unakamilika kwa wakati na ubora unaotakiwa kwani maendeleo yake hayaridhishi

Dr Mollel ameyasema hayo katika ziara ya ghafla aliyoifanya hapo jana katika Hospitali hiyo ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi na kusema kuwa Ujenzi wa Hospitali hiyo unasuasua huku sababu za Msingi za kutokamilika kwa mradi huo wenye zaidi ya miaka mitano zikiwa changamoto.

Hivyo Naibu Waziri wa Afya Mollel ametoa angalizo kwa wasimamizi wa Ujenzi wa mradi huo kuhakikisha unakamilika kwa wakati na ubora unaotakiwa na baada ya wiki mbili atarudi Mkoa wa Katavi kukagua Maendeleo ya Ujenzi huo.


Naibu Waziri wa Afya Dr Godwin Mollel akiwa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi

Sambamba na hayo Dr Mollel amesema kukamilika kwa Hospital ya Rufaa Mkoa wa Katavi itapunguza kiasi Cha fedha zaidi ya Tshs Milioni 200 zilizokuwa zikitengwa kwa ajili ya gari ya wagonjwa (Ambulance) ilikuwapeka wagonjwa Mikoa ya Mbeya na Mwanza kwa ajili ya kutibiwa.

Ameeleza kuwa baadhi ya wagonjwa wengine waliokuwa wakipatiwa Rufaa kwenda kutibiwa nje ya Mkoa wa Katavi, Rufaa hizo zilikuwa hazina sababu kwani magonjwa hayo yangeweza kutibiwa hapa hapa katika Hospitali ya Mkoa wa Katavi.
 
Mbali na kutoridhishwa na kasi ya Ujenzi wa Hospitali hiyo ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi Naibu Waziri wa Afya Mollel hakusita kuupongeza Uongozi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Katavi kupitia kwa Mkurugenzi wake Yusta Tizeba kwa kufanya vizuri katika huduma ya kutoa Chanjo dhidi ya Uviko 19 kwani Mkoa wa Katavi umeshika nafasi ya  tatu.

Dr Mollel pia alitembelea Chuo Cha Afya Mpanda na kukutana na wauguzi wa Afya ndani ya Mkoa wa Katavi pamoja na wanafunzi wanaosoma Chuoni hapo na kuwataka kufanya kazi pamoja na kusoma kwa bidii kwani Rais wa JMT Samia Suluhu Hassan ameipendelea Sana Sekta ya Afya hivyo wasimwangushe Rais badala yake wajitume kwa moyo kuwatumikia wananchi wa Katavi na Tanzania kwa ujumla.

Wanachuo wa Chuo Cha Afya Mpanda wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri wa Afya Dr Godwin Mollel alipotembelea Chuo hicho


Mkuu wa Chuo Cha Afya na Sayansi Shirikishi Mpanda Lightness Michael hakusita kumshukuru Naibu Waziri wa Afya Dr Mollel kufika Chuoni hapo na kumwomba Chuo hicho kuongezewa kozi ya uuguzi kwani wanakozi moja tu ya Famasia sambambana na kueleza changamoto ya vyumba vya madarasa vinavyokabili Chuo hicho na kumwomba angalau kwa kuanzia ongezeko la vyumba vya madarasa sita.

Naibu Waziri wa Afya Godwin Mollel hakusita kupokea ombi hilo na kuahidi kulifanyia kazi ikiwa ni pamoja na kutoa kipaumbele kwa watumishi wa Afya kutoka katika Mikoa  iliyopo pembezoni Kigoma, Ruvuma pamoja na Katavi kwenda kusoma ili Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Katavi itakapokamilika iwe na madaktari bingwa kwa ajili ya kutoa huduma nzuri na bora kwa wakazi wa Mkoa huo.

Nae Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Katavi Beda Katani hakusita kumsihi Naibu Waziri Dr Mollel kufuatilia endapo kuna namna yoyote inayokwamisha kukamilika kwa Hospitali hiyo ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi kwani kukamilika kwake kutasaidia sio tu wakazi wa Mkoa wa Katavi pia nchj jirani za Kongo na pia wagonjwa wa Rufaa watapungua na kupunguza gharama zilizokuwa zikitumika kuwasafirisha .


Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Katavi Beda Katani (wa kwanza kushoto), Naibu Waziri wa Afya Dr Godwin Mollel (wa pili kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Onesmo Busweru ambaye anakaimu nafasi ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi pamoja Mkuu wa Wilaya ya Mpanda



Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages