Baadhi ya Waandishi wa Habari waliopoteza maisha leo January 11,2022 katika ajali iliyotokea eneo la Busega
Simiyu
Taarifa kamili juu ya ajali iliyohusisha waandishi wa habari Mkoa wa Mwanza.
............................................
Ndugu Waandishi wa Habari na wadau wa habari , asubuhi ya leo tuliwataarifu taarifa ya awali juu ya ajali ya waandishi wenzetu wa Mkoa wa Mwanza.
Baada ya kufika kwenye Zahanati ya Busenga nilipewa jukumu la kuwataambua marehemu.
Waliofariki ni
1.Husna Milanzi - ITV
2.Johari Shani - Uhuru Digital
3.Antony Chuwa - Habari Leo Digital
4.Abel Ngapenda - Afisa Habari ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mwanza
5.Steven Msengi - Afisa Habari Ukerewe.
Majeruhi.
1.Tunu Hermany - Freelancer Journalist
2 Van Charles - Icon TV
Kwa sasa tupo njiani na miili ya wapendwa wetu kuelekea hospitali ya Mkoa ya Seketoure Mwanza.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Simiyu chanzo cha ajali ni mwendo kasi wa magari yote mawili na amethibitisha vifo hivyo.
Taarifa nyingine za uratibu wa msiba tutawajuza.
Mwanza press club tumepokea kwa masikitiko makubwa msiba huu.
Kazi ya Bwana haina makosa, jina lake lihidimiwe.
Edwin Soko
Mwenyekiti
Mwanza Press Club
11.01.2022