WANAFUNZI ZAIDI YA LAKI 2 KUNUFAIKA NA VICHUJA MAJI KUTOKA KAMPUNI YA KT&G YA KOREA KUSINI

  


 Mmoja wa Wanafunzi wa Shule ya Msingi Mtande Wilayani Chunya Mkoa wa Mbeya akitumia moja ya kifaa cha kuhifadhia maji kilichotolewa na kampuni ya  KT&G  shuleni hapo.


Walter Mguluchuma

Chunya,Mbeya

KAMPUNI kutoka Korea ya Kusini imetoa msaada wa vichuja na vitakasa maji vyenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 240 ambao utanufaisha  wanafunzi 260,000 nchini.

 Kampuni hiyo ya KT&G  inayonunua na kusafirisha tumbaku nchini kwenda nchi za Asia mbali ya  kuwapa wanafunzi maji safi na salama pia inahifadhi mazingira kwa kuwa uendeshaji wake hautumii nishati yoyote ya asili kama kuni na makaa ya mawe.

Akizungumza kwa niaba ya kampuni hiyo,Mike Costa alisema mwezi Machi mwaka jana kampuni hiyo ilichagua Shule ya Msingi Mtande ambapo  hafla ya mapokezi ya vifaa hivyo  na sherehe za kukabidhi vifaa hivyo ilifanyika Desemba 16 mwaka jana.

Aliongeza kuwa biashara ya tumbaku ndiyo inaongoza katika bidhaa zinazosafirishwa kutoka Tanzania kwenda Korea ya Kusini na kampuni ya KT&G imefunga mkataba wa kununua tani za tumbaku 2,850 kwa mwaka 2021 pekee. 

Aliendelea kusema KT&G uamuzi wa kugawa vichuja na vitakasa maji ili kulinda afya za wanafunzi  wadogo Tanzania ni kuakisi sera yake ya haki za binadamu na uhifadhi wa mazingira.

" Msaada huu  utawafikia wanafunzi 260,000 ambao watakuwa na  uhakika wa maji safi na salama kiasi cha takribani lita 340,000,000  kwa sababu vichuja maji hivi havitumii kuni Wala mkaa na v8itachangia kupunguza kiasi cha tani 13,000 za hewa ukaa hali ambayo itasaidia kuhifadhi mazingira" alisisitiza

Aliongeza kuwa kwa kushirikiana na “Water and Life” KT&G imechagua shule za msingi 300 kwenye mazingira na Wilaya zinazolima tumbaku na kugawa kiasi cha viafaa 1,300 vya kuchuja na kutakasa maji.

Alisema Kampuni ya KT&G imeanzishwa miaka 100 iliyopita, Kimataifa kampuni hii ni kati ya kampuni tano bora na bidhaa ya kwanza itokanayo na tumbaku ni essie na kwa sasa kampuni inajitanua kibiashara na kuzalisha “red ginseng”, madawa na bidhaa za urembo miongoni mwa vingine vingi.

"Ugharamiaji wa misaada unafanywa kwa asilimia 100  na Mfuko wa Sangsang,mfuko ambao unakusanya michango ya hiari toka kwa watumishi wa kampuni kupitia mishahara yao na baadae kampuni inachanga kiwango sawa na kilichohangiwa na watumishi"alisisitiza.

Mkuu wa Shule ya Msingi Mtande,Salumu ambaye alihudhuria mabidhiano hayo aliishukuru kampuni ya KT&G kwa msaada huo uliotolewa shuleni kwake na alishukuru kwa kuwa sasa wanafunzi wa shule yake wanakunywa maji Safi na salama na kuwa ni matarajio yake kampuni ya KT&G itaendelea kuwasaidia.


Picha ya Viongozi wa Kijiji cha Mtande Wilaya ya Chunya wakiwa na Waalimu wa Shule ya Msingi Mtande pamoja na Mwakilishi wa kampuni ya ununuzi wa Tumbaku ya PREMIUM wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya (mwenye suti)baada ya kupokea  msaada wa vichuja na vitakasa maji uliotolewa  na kampuni ya KT&G  kwa ajili ya shule ya Shule hiyo.(Picha na Walter Mguluchuma)

PICHA ZA MATUKIO MBALIMBALI WAKATI KAMPUNI YA KT&G IKIKABIDHI MSAADA WA VIFAA VYA KUTUNZIA  MAJI VYENYE THAMANI YA Tsh MILIONI 240 KATIKA SHULE YA MSINGI MTANDE WILAYA YA CHUNYA MKOA WA MBEYA.


BAADHI YA WATUMISHI WA KAMPUNI YA KT&G WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA

BAADHI YA WANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI MTANDE WAKICHUKUA MAJI YA KUNYWA  KATIKA MOJA YA KIHIFADHI MAJI WALICHOPATIWA SHULENI HAPO NA KAMPUNI YA KT&G



WANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI MTANDE WAKIWA NA GLASS ZA MAJI BAADA YA KUCHUKUA KWENYE KIHIFADHI MAJI KINACHOONEKANA PEMBENI KULIA KILICHOTOLEWA NA KAMPUNI YA KT&G

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages