RC MRINDOKO AHIMIZA WANAWAKE KUCHANGAMKIA FURSA YA KILIMO

 

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko (wa kwanza kulia )akitembelea shamba la mfano la zao la pamba.

Na Frida Gonzi.

MKUU wa Mkoa wa Katavi,Mwanamvua Mrindoko amewashauri wanawake wa mkoa huo kuchangamgikia fursa ya kilizo cha zao la pamba ili kuongeza kipata chao na taifa kwa ujumla.

Mkuu wa Mkoa huyo ametoa kauli hiyo jana katika kijiji cha Kaseganyama halmashauri  ya wilaya ya Tanganyika Mkoani humo ambapo amewasisitiza wanawake kutokubaki nyuma kwenye kuchangamkia fursa zinazopatikana kwenye kilimo.

Mrindoka amesema kuwa kuna dhana potovu kwa baadhi ya watu wa jamii ya mkoa huo kubagua baadhi ya kazi kuonekana kama zinawahusu wanaume pekee yao na kuna baadhi ya kazi zinawahusu wanawake pekee.

Amewaambiwa wanawake kuachana na dhana hiyo potovu kwa sababu serikali inasera  nzuri ambazo zitamsaidia mwanamke kujikwamua kiuchumi.

" serikali inatoa mikopo kwa wanawake,vijana na watu wenye ulemavu huo ni uwanda mpana sana unaowawezesha wanawake kujipatia fedha kwa riba nafuu...sasa wanawake wezangu chukue nikopo hiyo na leteni kwenye uzalishaji wa zao wa kilimo cha pamba" Amesema Mrindoko.

Amesema zao la pamba ni dhahabu nyeupe ambapo kama jamii itaamka hususani wanawake ambao ndio wazalishaji wakubwa kwenye nganzi ya familia watafanikiwa kwa ukubwa zaidi kuimarisha vipato vyao.

"Kama mtaweka mipango mizuri kwenye kilimo cha pamba hamtaweza tena kuuza mahindi kama zao la biashara" Amesema Mkuu wa Mkoa huyo ambapo amesisitiza jamii kuacha tabia ya kuuza mazao ya chakula kama chanzo cha mapato

Naye Frida Masanja amemshukuru Mkuu wa Mkoa huyo kwa kuwapa hamasa kubwa ya kujihusisha na kilimo hususani cha pamba pia amemhakikishia kuwa hawatabweteka kuwategemea waume zao.

Frida amesema kuwa mikopo wanayopatiwa kwenye halmashauri wataweza kuiwekeza kwenye kilimo ili kuweza kuongeza uzalishaji wa kilimo na kujipatia fedha ambazo zitawasaidia kurejesha mikopo hiyo kwa wakati pamoja na kujikwamua moja kwa moja kiuchumi.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages