AJINYONGA CHUMBANI KWA MPENZI WAKE

 

Picha ya  Fuvu alilofukua Marehemu kabla ya kujinyonga kwenye makaburi yaliyopo Mwangaza na kwenda kulitupa dukani kwa Ndugu yake tukio lililozua taharuki Mtaa wa Mpanda  Hotel siku ya Jumamosi February 12,2022
 
Na  Walter Mguluchuma

    Katavi

Mkazi wa Mpanda Hotel Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi Wille Mwakapimba  amekutwa akiwa amejinyonga chumbani  kwa mpenzi wake Hawa Ayubu  na kuacha ujumbe uliyoandikwa kuwa alisikia ujumbe wa sauti ya Mama yake ambae ni marehemu  ikimtaka aende  kufukua kaburini  lake(mama yake)lililopo makaburi ya Mwangaza  kuna vitu vya kishirikina vimefukiwa kwenye kaburi hilo.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Kivukoni  Kata ya Shanwe Michael Sikenyenzi amesema kuwa tukio la mtu huyo kujinyonga limetokea jana majira ya saa nne na robo  huko Kata ya Shanwe Manispaa ya  Mpanda  muda mfupi baada ya marehemu kutoka kituo cha Polisi Wilaya ya Mpanda .

Alisema kuwa taarifa za tukio hilo alizipata baada ya kupigiwa simu iliyomtaka kwende nyumbani kwa  Hawa Ayubu  kuna tukio la mtu kujinyonga nyumbani kwa mwanamke huyo .

Amebainisha kuwa  baada ya kufika nyumbani kwa Hawa alikuta mwili wa marehemu  huyo akiwa amejinyonga chumbani hali iliyomlazimu kutowa taarifa  Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi ambao walifika haraka eneo la tukio.

Sikenyenzi aliongeza kuwa baada ya Polisi kufika eneo la tukio waliingia chumbani na kukuta ujumbe wa maandishi aliokuwa ameandika marehemu ambao ulikuwa ukieleza kuwa  alisikia sauti ya marehemu mama yake aende kwenye kaburi lake(marehemu mama yake)akafukuwe kuna vitu vimefukiwa na ndugu yake ambae amekuwa akiwafanyia ushirikina ndugu zake .

Alisema  baada ya kusoma barua hiyo waliwahoji ndugu wa marehemu waliokuwa wamefika kwenye eneo hilo akiwepo Kaka yake Mkubwa wa marehemu  ambae alidai kuwa ni kweli marehemu huyo alikwenda kwenye makaburi ya Mwangaza  na kufukua na kukuta kichwa  kinachosadikiwa cha binadamu na sehemu ya siri ya mwanamke sanda na kitambaa chekundu ambavyo alivichukuwa na kuvipeleka dukani kwa ndugu yake aliyekuwa akimtuhumu kuwa ni mshirikina .

Alieleza kuwa baada ya kuwa amevipeleka vitu hivyo hapo  Februali 11 kwenye duka hilo lililopo Mtaa wa Mpanda Hoteli  Polisi walipata taarifa ya tukio hilo na walimkamata marehemu huyo na kumweka  mahabusu hadi  siku iliyofuata mchana .

Amefafanua kuwa kabla ya marehemu kufanya kitendo hicho cha kujinyonga alikuwa ametokea kituo cha Polisi  Wilaya ya Mpanda alipokuwa amekwenda kuripoti kama ambavyo alikuwa ametakiwa na Jeshi hilo .

Mke wa Marehemu huyo  Hawa  Ayubu alisema kuwa  yeye na marehemu walikuwa wakiishi kama mume na mke kwenye nyumba ambayo aliachiwa na mume wake ambae alifariki dunia na kumwachia nyumba hiyo ambapo kwenye maisha yake na Wile wamefanikiwa kuzaa mtoto mmoja wakike.

Amesema  kuwa yeye alipigiwa simu na mume wake huyo ambae alimtaka awahi kurudi nyumbani kwamba alikuwa na shida nae ndipo alipofika nyumbani na kuingia ndani ya  chumba walichokuwa wanalala alimwona mumewe akiwa ananing'inia juu ya paaa la nyumba kwa kutumia kamba huku pembeni kukiwa na situli pembeni ya kitanda .

Mmoja wa majirani  Anastazia John anashuhudia kuwa walisikia mayowe ya  Hawa Ayubu akipiga kelele ya kuomba msaada  hali ambayo iliwalazimu wao majirani wafike kwenye eneo hilo na walipofika ndani ya chumba walikuta mwili wa marehemu ukiwa juu ya paa ya nyumba huku akiwa amejinyonga na mkewe akiwa amepoteza fahamu kutokana na mshituko wa kifo cha mume wake .

  

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages