HATIANI KWA KUKAMATWA NA MENO YA TEMBO MKOA WA KATAVI


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi ACP Ali Makame Hamad akionyesha jino la Tembo kwa Waandishi wa Habari ofisini kwake walilolikamata katika doria na misako inayoendelea katika Mkoa wa Katavi

Na Irene Temu
Katavi

Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi linamshikilia Beno Martias(68)Mkazi wa Ibindi na Nova Issaka (45) Mkazi wa Itenka A wakiwa na meno mawili ya tembo katika Tarafa ya Nsimbo Wilaya ya Mpanda.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi ACP Ali Makame Hamad amesema kuwa mnamo February 10,2022 katika Kijiji Cha  Itenka A Jeshi la Polisi liliwakamata watuhumiwa hao na meno mawili ya tembo yakiwa ndani ya mfuko wa sandalusi wakiyasafirisha kwa kutumia pikipiki yenye namba za usajili MC.410 BQW aina ya Sanlg.


Pikipiki iliyokuwa 
Ikisafirisha meno ya Tembo

Na kwamba upelelezi wa tukio hilo unaendelea na watuhumiwa watafikishwa Mahakama pindi upelelezi utakapokamilika kujibu tuhuma zinazowakabili.

Sambamba na hayo Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi linamshikilia Joseph Paulo (27)Mkazi wa Nsemulwa na Mwalimu wa Mafunzo ya dini kwa kulawiti watoto wanne ambao majina yao yamehifadhiwa.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi ACP Ali Makame Hamad ameeleza kuwa mtuhumiwa huyo alikuwa akiwarubuni wahanga hao kwa kuwabeba kwenye pikipiki yake huku akiwaambia wamsindikize kwenda kufanya shughuli zake za kibiashara sehemu mbalimbali.

Na ndipo kila baada ya  kumaliza vipindi vyao vya masomo ya dini alikuwa akiwachukua na kwenda kuwafanyia vitendo vya kikatili kwa kuwalawiti kwa nyakati tofauti tofauti.

Hivyo mtuhumiwa yatari amekwisha fikishwa Mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria.

Kutoka na tuko hilo Kamanda Hamad ametoa wito kwa wazazi na wakazi wote wa Mkoa wa Katavi kuwa makini na kufuatilia mienendo ya watoto wao pindi wawapo shuleni hata sehemu nyingine wanazo wapeleka kwa ajili ya kujifunza na kuhakikisha watoto wao wanakuwepo nyumbani muda unaostahili.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages