ENEO LA MAZIKO LARUDISHWA KWA WANANCHI


Baadhi ya Wananchi wa Mtaa wa Msasani Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi  wakifanya usafi kwenye makaburi ya Msasani ambayo walikuwa wamezuiliwa kutumia kwa ajili ya maziko  toka Mwezi wa Sita Mwaka Jana kwa kile kilichodaiwa kuwa makaburi hayo yapo  ndani ya eneo la Jeshi la Wananchi wa Tanzania kwa sasa wananchi hao kuanzia Februari 20,2022 Jeshi la Wananchi limewarudishia wananchi kufanyia maziko.(Picha na Walter  Mguluchuma)

Na Walter MguIuchuma

 Katavi .

 Wananchi wa Mtaa wa  Msasani katika  Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi wamelishukuru Jeshi la Wananchi wa Tanzania kwa kuwaruhusu kuendelea kufanya mazishi katika makaburi ya Msasani ambayo Jeshi hilo lilikuwa limezuia toka mwaka jana  kufanyia mazishi kwenye makaburi hayo ambayo yamekuwa yakitumika toka mwanzoni mwa 1970.

 Mwenyekiti wa Mtaa huo  Juvenali  Deus alisema kuwa toka mwaka jana mwezi wa sita wananchi wa Mtaa huu  wamekuwa wakihangaika kutafuta maeneo ya kufanyia mazishi kufuatia eneo walilokuwa wakifanyia mazishi kuzuiwa na Jeshi la wananchi licha ya  kuwa makaburi hayo yalikuwa yakitumika kwa ajili ya mazishi kwa kile kilichokuwa kinadaiwa na Jeshi la wananchi .

Hali hiyo ilikuwa ikiwalazimu mtu akifariki kwenda kuomba  kuzikwa kwenye maeneo ya Kata ya Ilembo na Mpanda Hoteli ambako kulikuwa ni mbali na eneo hilo ambalo wananchi hao walikuwa wamelizowea kuliko kwenye makaburi ya Kata hizo zilizo mbali na mtaa huo .

Amebaisha wananchi hao ambao ni zaidi ya mia tano muda wote huo wamekuwa wakitowa kilio chao kwa Uongozi wa Serikali ya Wilaya ya  Mpanda  na Mkoa wa Katavi  wakiomba warejeshewe makaburi hayo ambayo wamezikwa ndugu zao wapendwa   .

 Mwenyekiti huyo wa Mtaa  Juvenali Deus amesema kuwa kutokana na kilio hicho cha wananchi Jeshi la Wananchi limeridhia kuanzia tarehe 20 mwezi huu wananchi kuendelee  kutumia tena makaburi hayo ambayo yapo kwenye eneo la jeshi la wananchi .

Hivyo wamelishukuru Jeshi la Wananchi kwa kuwarudishia eneo hilo na kuwaongezea tena eneo jingine lenye ukubwa wa Ekali tano na  zaidi ya lile eneo walilokuwa wakilitumia kabla ya kuzuiwa kufanyia mazishi .

Nae Abdula Azizi  Mkazi wa Mtaa huo amesema wanashukuru kwa uamuzi huo kwani walikuwa wakiipata shida pale inapotokea mtu amefariki  kwani walikuwa wakihangaika sehemu ya kumsitiri.

Anaishukuru Serikali na Jeshi la Wananchi wa Tanzania  kwa sasa wanauhakika wa eneo la kufanyia maziko tofauti na ilivyokuwa hapo awali walivyokuwa wamezuiliwa kufanyia mazikonkwenye makaburi hayo .

Joseph  Pascal  amesema kuwa licha ya maeneo hayo kurudishwa kwa wananchi ameomba kuwa kuna baadhi ya maeneo wanayoishi ambayo yako nje ya makaburi yanayosadikiwa kuwa ni ya Jeshi la Wananchi wanaiomba Serikali ifanye utaratibu wa kuyarudisha kwa wanachi ili waendelee na shughuli zao za uzalishaji mali .

Kwa upanda wake Rehema Mstaphar  alisema kuwa walikuwa wanasikitika sana na kuwaza kukosa sehemu za kufanyia mazishi kwani walikuwa wakijua hizo ndio nyumba zao kubwa za milele walipata shida ya kuwahifadhi ndugu zao wanapokuwa wamefariki wanawashukuru watu wa maeneo mengine ambao kwa kipindi hicho waliwaruhusu kuzikia kwenye makaburi yao.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages