MILIONI 42 ZATOLEWA NA SIDO KWA WAJASIRIAMALI MKOA WA KATAVI


Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Onesmo Busweru ambaye pia ni Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Mpanda akikabidhi hundi za malipo kwa Wajasiriamali waliopatiwa mkopo kutoka  Sido


Na Paul Mathias

Katavi

Shirika la kukuza Viwanda vidogovidogo Sido Mkoa wa Katavi limewakopesha  Wajasiriamali shilingi Milioni 42 katika Mpango walionao katika Shirika hilo lengo likiwa ni kuwa kwamua kiuchumi.

Hayo yamebainishwa na Kaimu Meneja wa Sido Mkoa wa Katavi Salome Mwasomola wakati wa hafla ya kukabidhi Mikopo hiyo ambapo amesema Sido imeanza kutekeleza Mpango huo kwa vitendo kwa kutoa Mikopo hiyo na Wajasiriamali wapatao 48 tayari  wamenufaika na  mpango huo.

Awali akitoa neno kwa Wajasiriamali hao Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Onesmo Buswelu amesema Serikali imekuwa ikiandaa mazingira wezeshi kwa Wajasiriamali kwa kuja na mipango mbalimbali ya kuwajali ili wajikwamue kiuchumi na kuwaomba kutumia Mikopo hiyo kwa malengo yaliyo kusudiwa.

Kwa upande wao Wajasiriamali hao wamesema Mikopo hiyo itawasadia katika kuimarisha shughuli zao kwa kuwa haina riba na kuishukuru serikali kwa kuja na mpango huo kupitia Shirika hilo la Sido.

Mjasiriamali akipokea hundi ya malipo ya mkopo kutoka Sido kwa Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Onesmo Busweru


Licha ya serikali kuendelea kutoa mikopo kwa makundi ya wanawake walemavu na Vijana bado imeendelea kwa kuweka mpango wa kutoa Mikopo kwa Wajasiriamali kupitia Shirika la Sido.

Wajasiriamali wa Mkoa wa Katavi wakiwa katika hafla ya kukabidhiwa hundi za malipo ya mkopo kutoka Shirika la Viwanda vidogovidogo(SIDO) Mkoa wa Katavi


Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages