![]() |
| Mkurugenzi mkuu wa bodi ya Tumbaku Tanzania Stanley Mnozya akielezea mkakati wa bodi ya Tumbaku kwa makampuni ya ununuzi wa zao hilo . |
Na Walter Mguluchuma-Katavi
Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Tumbaku Tanzania Stanley
Mnozya ameyaagiza
makampuni yote yanayonunua
Tumbaku kwa wakulima kuhakikisha yanafuata
kanuni na taratibu ya kulipa fedha za wakulima kwa wakati huku akionya kampuni
ambazo zitashidwa kufanya hivyo zitachukuliwa hatua kali za kisheria.
Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Tumbaku Tanzania Stanley Mnozya ameyaagiza makampuni yote yanayonunua Tumbaku kwa wakulima kuhakikisha yanafuata kanuni na taratibu ya kulipa fedha za wakulima kwa wakati huku akionya kampuni ambazo zitashidwa kufanya hivyo zitachukuliwa hatua kali za kisheria.
Hatua
hiyo ya Bodi ya Tumbaku imechukuliwa
kufatia kuwepo kwa malalamiko kwa baadhi ya Amcos hapa nchini ikiwepo KASI AMCOS ya Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi kuchelewechewa
malipo yao na baadhi ya Makampuni
.
Mnozya amesema
alipokuwa Katavi alikutana na kesi kwamba chama cha Msingi Kasi kilikuwa hakija lipwa fedha zao kiasi cha Dolla Zaidi ya 312 000 na kampuni moja ya ununuzi
wa zao la Tumbaku .
Kufatia
changamoto hiyo yeye Mkurugenzi Mkuu wa bodi ya Tumbaku aliwahidi wakuluma hao
kuwa atashughulikia changamoto yao na
tayari wakulima hao kulipwa fedha zao zote
na kufanya Mkoa wa Katavi
wakuluma wake wote kulipwa kiasi cha shilingi Bilioni 120 na kwa sasa hakuna mkulima ambae anadai
fedha yoyote ile .
Mnozya ameziagiza Kampuni zote zinazo nunua zao la Tumbaku hapa nchini kuhakikisha zinafuata sharia kanuni na taratibu zinapokuwa zimenunua tumbaku ya wakuluma zilizopo na wasichelewesha malipo ya wakuluma kufanya hivyo ni uvujanji wa sharia zinazosimamia zao hilo .
Ameyaonya
makampini yote yanayonunua Tumbaku hapo nchini kwa msimu ujao yatakayo jaribu
kuwachelewesha wakuluma hatua kali sana za kisheria zitachukuliwa dhidi yao .
Mnozya
amesisitiza kuwa kitendo cha kuwachelewechea malipo ni kuwahuhumu wakuluma kwani mkulima amelima ilia pate fedha
aweze kujenga nyumba .kulipia ada za watoto shule na pia grarama za
matibabu na mahitaji mengine mbalimbali
ya maendeleo .
Hivyo
unapomcheleweshea unamrudisha nyuma
maendeleo yake hivyo makapuni
yahakikishe yanajipanga vizuri kuona namna
ya kuwalipa wakuluma kwa wakati .
Amewaasa
wakulima wauze tumbaku pindi Bodi ya Tumbaku inapokuwa imetangaza
kuanza masoko mwezi wan ne au watano
kwani kipindi hicho tumbaku inakuwa na
uzito na ubora na wakuluma wanapata fedha za kitosha .
Lamack
Mbuza mkulima wa Amcos ya Kasi amesema
kwa msimu huu wamepitia katika kipindi kigumu sana kufutia kampini ya Magefa kuchelewa kuwalipa
fedha zao hadi jitihada
kubwa zilizofanywa na Mkurugenzi wa Bodi ya Tumbaku na timu yake ndio
wameweza kulipwa hivi karibuni fedha zao zote ,
Makamu
Mwenyekiti wa Amcos ya Kasi Gerald Kipanta
ameyaomba makampuni yanayonunua zao
la Tumbaku kuwa na utaratibu wa kuwalipa wakulima mapema .
