| Picha na Mtandao |
Na Walter Mguluchuma
Katavi .
Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi linamshikilia Alex Kasambe Mkazi wa Tambukareli Manispaa ya Mpanda kwa kumakamata na dawa za kulevya aina ya bangi debe mbili akiwa ameficha ndani ya chumba chake anachoishi .
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi All Makame Hamad amewaambia Waandishi wa Habari mtuhumiwa huyo alikamatwa Machi 12 majira ya saa sita usiku huko katika Mtaa wa Tambukareli alikokuwa akiishi .
Alisema mtuhumiwa alikamatwa kufutia Jeshi hilo la Polisi kupata taarifa za mtumiwa huyo kuwa ana jihusisha na biashara ya kuuza dawa za kulevya aina ya bangi .
Baada ya Jeshi hilo kupata taarifa lilianza kufanya uchunguzi na ndipo baada ya kukamilisha uchunguzi walifanikiwa kumkamata mtuhumiwa Alex Kasambe akiwa na debe mbili za bangi .
Kamanda All Makame Hamad ameeleza kuwa mtuhumiwa huyo alikamatwa akiwa amehifadhi bangi hiyo debe mbili katika mfuko wa sandarusi huku akiwa ameificha kwenye chumba chake cha kuishi .
Mtuhumiwa bado anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa mahojiano zaidi kwa lengo la kupata mtandao mzima wa kuwapata watuhumiwa wengine ambao wamekuwa wakijihusisha na biashara hiyo haramu.
Upelelezi utakapo kamilika mtuhumiwa Alex Kasembe atafikishwa mahakamani ili kujibu tuhuma inayomkabili ya kupatikana na debe mbili za dawa za kulevya aina ya bangi .
Aidha Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi amewapongeza wananchi wanaojitowa kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kuwapatia taarifa za uhalifu zinazosaidia kuuweka Mkoa wa Katavi kuendelea kuwa salama.