MAAFISA UGANI 10 WAPATIWA PIKIPIKI MKOA WA KATAVI


Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko akimkabidhi Mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda Sophia Kumbuli funguo ya pikipiki za Maafisa Ugani wa Idara ya Mifugo Ishara ya kuzipokea kwa niaba ya Wakurugenzi wengine wa Halmashauri zote za Mkoa wa Katavi.

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko ikiwasha moja ya pikipiki Kati ya pikipiki 10 zilizotolewa kwa Maafisa Ugani  Idara ya Mifugo katika Halmashauri zote za Mkoa wa Katavi Ishara ya kuzizindua na kuwaasa Maafisa Ugani hao kuzitumia kwa matumizi ya Serikali na sio binafsi(bodaboda)

Afisa Mifugo Halmashauri ya Nsimbo
Daniel Walakunga akipokea funguo ya pikipiki kutoka kwa Mkuu wa Mkoa Mwanamvua Mrindoko na kushukuru kwa kupatiwa vitendea kazi hivyo aina ya pikipiki na kuahidi kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.
Veronica Mgina Afisa Ugani kutoka Halmashauri ya Mpimbwe kata ya mamba akipokea pikipiki kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi na kuahidi kufanya kazi kwa weledi na kuongeza tija katika Halmashauri zao.

Afisa Mifugo Manispaa ya Mpanda  Tulinao Nswila akipokea funguo ya pikipiki kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko zilizotolewa na Idara ya Mifugo lengo likiwa ni kuongea tija katika Sekta ya Mifugo na kuwafikia wafugaji na wakulima popote walipo na kutumia utaalam wao.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages