PIKIPIKI ZITUMIKE KWA KAZI ZA SERIKALI SIO BINAFSI


Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko(kulia)akiwa na Afisa Mifugo Mkoa wa Katavi(katika) Zidihery Mhando wakiwasha pikipiki yatari kuwakabidhi Maafisa Ugani Idara ya Mifugo katika Halmashauri zote za Mkoa wa Katavi.

Na Irene Temu

Katavi

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko amekabidhi pikipiki 10 kwa Maafisa Ugani Idara ya Mifugo katika Halmashauri zote za Mkoa wa Katavi na kuwaasa kuzitumia kwa matumizi ya Serikali na sio binafsi huku akisisitiza zikalete tija katika Sekta ya Mifugo.

Mkuu wa Mkoa Mwanamvua ameyasema hayo wakati akikabidhi pikipiki hizo kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda Sophia Kumbuli kwa ajili ya kuwapatia maafisa Ugani kwa niaba ya Wakurugenzi wa Halmashauri nyingine waliokuwa katika shughuli nyingine za kitaifa tukio lililo fanyika nje ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.

Aliwataka Maafisa Ugani hao kutumia pikipiki hizo kwenda kutoa Elimu kwa wafugaji na wakulima pamoja na kutatua migogoro baina ya wafugaji na wakulima kutokana na muingiliano baina yao.

".. mfugaji na mkulima wanakutana sehemu moja pale mfugaji anapopitisha Mifugo yake kwenda kula nyasi na kunywa Maji katika shamba la mkulima ambaye amepanda mazao mbalimbali katika shamba lake hapo ndio migogoro inapoanza"alieleza Mkuu wa Mkoa Mwanamvua

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko(kulia)baada ya kumkabidhi Mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda Sophia Kumbuli(kushoto)funguo za pikipiki kwa Niaba ya Wakurugenzi wa Halmashauri zote za Mkoa wa Katavi

Hivyo kwakupata vitendea kazi hivyo aina ya pikipiki amewataka Wataalam hao kwenda kuhakikisha Migogoro hiyo inatatuliwa na kumalizika kwa kutumia utaalam wao na kuhakikisha wanawasimamia vizuri wafugaji kwa kuwapa maeneo yaliyotengwa kwa matumizi Bora ya ardhi na kuwaongoza kupata nyasi bora na kubadilisha Sekta ya Mifugo kuwa yenye tija.

Wakurugenzi wametakiwa kusimamia vyombo hivyo vya usafiri kufanya kazi za Serikali na sio kazi binafsi na pikipiki hizo zikawe mwanzo wa kuona tija ya ufugaji katika Sekta ya Mifugo ndani ya Mkoa wa Katavi.

Pia Maafisa Ugani wameonywa kutumia pikipiki hizo kwa kukodisha au kufanya kazi zao binafsi badala yake zitumike kufanya kazi za Serikali.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages