![]() | |
|
Wanawake wa Mkoa wa Katavi wametakiwa kusimamia N-4 (N-Nne) kama Msingi wa maisha yao na Jamii inayowazunguka ambapo itawasaidia kwenye kusukuma juhudi za usawa wa kijisia katika jamii.
Wito huo umetolewa kwa wanawake na Daktari bingwa wa magonjwa ya watoto wa Hosptali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi,Dkt Yusta Tizeba kwenye hafla ya mwanamke wa thamani iliyofanyika kwenye ukumbi wa Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi.
Dkt Tizeba amesema kuwa N-Nne zinabeba dhima ya
Natabua,Najielewa,Najikubali na Najiamini ambapo ujumbe huo ni nguzo muhimu wa
kuhakikisha jamii inapaswa kutambua na kumpatia mwanamke fursa ya kuweza
kufanya kazi za kiuchumi,siasa na utawala kwa kuondokana na dhana potofu ya
kuwa mwanaume ndiye pekee mwenye uwezo wa kufanya hayo.
Amefafanua kuwa licha ya kuwepo kwa maazimio na sheria nyingi za kuhimiza usawa kwenye jamii,wanawake na wasichana kila kona ya dunia wanaendelea kuteseka,kunyanyasika na kuonewa na yote hayo ni kutokana na kuwepo kwa mizizi dume na uchu wa madaraka.
Amewaambia wanawake kuwa kwa mujibu wa shirika la umoja wa mataifa la mpango wa maendeleo duniani (UNDP),nusu ya watu duniani bado wanaamini kuwa wanaume ndio viongozi bora wa kisiasa kuliko wanawake,na zaidi ya asilimia 40 wanaamini kuwa wanaume ndio wasimamizi bora wa biashara kuliko wanawake.
" wanawake wenzangu kanuni za kijamii ambazo zinadhoofisha haki za wanawake ni hatari kubwa kwa jamii,na zinadhoofisha pia ukuaji wa maendeleo ya binadamu" amesema Dkt Tizeba.
Aidha licha ya kuwa zipo changamoto nyingi kama hizo,Lakini kuna hatua kubwa za kupongeza serikali kwa kupiga hatua kwenye suala la usawa katika uongozi tangu awamu ya sita ya rais Samia Suluhu Hassain kuingia madarasani ambapo licha ya kuwa sasa kuna rais wa jinsi ya mwanamke lakini kada mbalimbali wanawake wameweza kuaminiwa kuongoza.
Amesisitiza kuwa sasa wanawake wanapaswa kuamka na kwa kutembea na N-Nne haiwezi kutokea mwanamke kushindwa katika juhudi za kujikwamua kimaisha kwa ni suala la kujitabua kwa sababu serikali imeonesha nia njema ya usawa katika jamii.
Lea Gawaza,Mwanzilishi wa wazo la Mwanamke wa Thamani amesema
jamii ya Mkoa wa Katavi inapaswa kutambua kuwa juhudi za kujenga usawa wa
kijisia zinapaswa kufanywa na jamii yote ili kufanikisha usawa huo.
Gawaza ameeleza kuwa katika migogoro yote ambayo ya kuachana na siasa jumuishi yanaweza kuibua chuki ya wanawake na ubabe vitaimarika na kinyume na jamii zilizo imara na zenye ustawi.