![]() |
| Picha na Mtandao |
Frida Gonzi,Mpanda
MKAZI wa kijiji cha Kakese tarafa ya Misukumilo Manispaa ya Mpanda Mkoa
wa Katavi anayefahamika kwa jina moja Mungo amesombwa na maji wakati akivuka mto
kwenda mnadani huku akiwa amebaba zaidi ya fedha mil moja na laki tano.
Imetajwa kuwa chanzo cha
kusombwa na maji ni ubovu wa miundombinu ya barabara hususani ya kukosekana kwa
madaraja na makalvati imari imara yatakayowasaidia wananchi kuvuka kwa usalama
zaidi.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Mbugani
Kata ya Kakese, Boniface Sendelali amesema kuwa mtu huyo amesombwa na maji
hapo juzi majira ya saa mbili asubuhi kwenye eneo la mto unaounganisha
vijiji vya Kakese na Kijiji cha Itenka.
Amesema siku hiyo ya tukio
mtu huyo aliaga familia yake kuwa anakwenda kwenye mnada wa ng'ombe
katika Kijiji jirani cha Itenka kwa lengo la kwenda kununua ng'ombe na
aliondoka akiwa amebeba kiasi cha Tshs 6,680,000.
Amebainisha kuwa kwenye
msafara huo alikuwa ameambatana na wanakijiji wenzake ambao nao walikuwa
wakielekea kwenye mnada huo kwa lengo la kwenda kununua Mifugo.
Baada ya kuwa wameanza
safari yao kuelekea Kijiji cha Itenka walifika kwenye mto ambao
unaunganisha vijiji hivyo viwili na walikuta mto umejaa na maji yakiwa yanapita
kwa kasi kwenye mto huo.
Nao baadhi ya wananchi wa
kijiji cha Kakese,Mariam Rashid amesema kuwa serikali inapaswa kufanyia kazi
kero ya ubovu wa miundombinu ya barabara kwani kwa muda mrefu sasa inawapa
wakati mgumu kuvuka katika mto huo.
“Kifo hiki kimetusikitisha
sana.Sisi tukiwa wanawake ndio wahanga wakubwa wa ubovu wa barabara na ubovu wa
madaraja ambapo tunashindwa kuvuka wakati tukiwa kwenye majukumu yetu ya kila
siku hususani ya kwenda kuteka maji” Amesema Mariam.
Janeth Anthony ametoa wito
kwa serikali kuimarisha miundombinu ya barabara kwa sababu barabara ni nyenzo
muhimu sana kwenye kusafirisha bidhaa hasa za mazao ya kilimo kwani jamii yao
niya wakuluma.
“Diwani anapaswa kutambua tumemchangua sio kwa sababu ya kuboresha maisha yake.Haiwezekani vifo vitokee kwa sababu ya ubovu wa daraja” Amesema
Diwani wa Kata ya Kakese,Maganga Salaganda amesema taarifa za
kusombwa na maji kwenye mto huo zilifika kwa viongozi wa Kata ambao nao
walifanya juhudi za kuanza kumtafuta kwa mchana na usiku.
Amesema hadi sasa licha ya juhudi hizo kuendelea mtu huyo bado haja patikana na wameamua pia kushirikisha jeshi la jadi la sungusungu ambao hadi sasa wapo kwenye eneo hilo la mto wakiendelea kumtafuta.
