TCCIA YAWATAKA VIJANA KUCHANGAMKIA FURSA ZA KIUCHUMI KATAVI.


Hassanal Shabil Dalla Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara na Viwanda Mkoa wa Katavi (TCCIA

George Mwigulu na Paul Mathias

Katavi.

Vijana wa Mkoa wa Katavi wameaswa kuchangamkia fursa za kiuchumi za Kilimo,Ufugaji  pamoja na uwekezaji wa viwanda vidogovidogo ili kuwa chachu ya ukuaji wa uchumi wao na Taifa kwa ujumla.

Kutokana na Mkoa huo kuwa ni miongoni mwa mikoa inayojijenga  kwenye miundombinu ya barabara,reli  pamoja na usafiri wa anga sambamba na kutengeneza mazingira wezeshi kwa vijana kujikwamua kiuchumi.

Hassanal Shabil Dalla ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya wafanyabiashara na viwanda Mkoa wa Katavi (TCCIA) alibainisha hayo jana ofisini kwake wakati akizungumzia fursa za uchumi zilizopo na mazingira ya kufanyabiashara yaliyopo Mkoa wa Katavi.

Mwenyekiti huyo aliweka wazi kuwa vijana wengi wa Mkoa wa Katavi wamekuwa na tabia ya kuilalamikia serikali kwa ukosefu wa ajira huku wakishindwa kuwa wabunifu wa kufanya miradi chanya ya kibiashara.

“ …vijana wameshindwa kuwa wabunifu wanaishia kwenye biashara ya bodaboda na bajaji pekee ambazo kiuhalisia licha ya kuwaingizia kipato kidogo lakini imekuwa chanzo za ajali nyingi ambazo zimekuwa zikiwasababishia ulemavu wa kudumu na vifo” alisema Dalla.

Dalla aliwaomba vijana kubadili fikra zao kwa kujitokeza kwa wingi kufanya kilimo cha umwagiliaji,kufungua viwanda vidogovidogo vya kuchomelea vyuma ambavyo vinapatikana kwa bei nafuu madukani ambavyo vitawaingizia kipato kikubwa zaidi ya kuwa bodaboda pekee.

Kuhusu suala la uwekezaji  alisema bado kunachangamoto za kutokuwa na umeme wa uhakika ndani ya Mkoa wa Katavi  na hata unaopatikana gharama yake imekuwa kubwa zaidi na kuwa chanzo cha viwanda kufungwa.

Alieleza kama serikali itamaliza changamoto ya umeme kutakuwa na ongezeko kubwa la wawekezaji  Mkoa wa Katavi  ambapo kama wao TCCIA wanauwezo wa kushashiwi zaidi ya wawekezaji 50 kuja Katavi.

Naye Mwakilishi wa Meya Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi ambaye ni Diwani wa Kata ya Kashaulili,Magreth  Kitungulu(Mhaya) alisema kuwa fursa za mikopo kwa vijana zipo nyingi endapo vijana watajiunga kwenye vikundi vitakavyowafanya kuwa na sifa ya kukoposheka.

Aidha alishauri pia SIDO Mkoa wa Katavi ni sehemu ya kuwakwamua watu kiuchumi ni vema shirika hilo likajitangaza kupitia fursa wanazozitoa kwani wananchi wengi bado hawajui fursa zinazotolewa na SIDO.

Diwani wa Kata ya Majengo Manispaa ya Mpanda,Mstahiki Meya Mstaafu William Mbogo ameeleza kuwa kumekuwa na changamoto kubwa za urejeshaji wa mikopo hasa kwa vijana wa Manispaa hiyo.

Diwani wa Kata ya Majengo Manispaa ya Mpanda na Mstahiki Meya Mstaafu William Mbogo 


Kushindwa kurejesha mikopo hiyo kumekuwa chanzo cha kukwamisha juhudi za serikali za kuwa kwamua vijana kiuchumi na kutumia fursa hiyo kuwaomba kurejesha mikopo kwa wakati.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages