AJINYONGA KWA MKANDA WAKE WA SURUALI


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi ACP Ali Makame Hamad

Na Irene Temu

Katavi

Dereva wa pikipiki (bodaboda) Idrisa Salum Milundiko(24) Mkazi wa Nsemulwa amekutwa katika Kijiji cha Kasokola mashariki B Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi akiwa amejinyonga kwa kutumia mkanda wake wa suruali chanzo kikiwa ni msongo wa mawazo.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi ACP Ali Makame Hamad ameeleza kuwa mnamo April 8,2022 Idrisa Milundiko alitoweka nyumbani kwao na kuacha ujumbe mfupi wa maandishi uliokuwa ukisema"Kaka Mimi naenda kujinyonga kwani nina matatizo mengi na mwili wangu upelekwe kwa mjomba wangu aishie  makanyigio"alinukuu Kamanda Hamad

Alieleza baada ya hapo Marehemu hakuonekana tena hadi alipokutwa akiwa amejinyonga porini majira ya saa saba na nusu mchana April 13,2022 eneo la Kasokola

 Mwili wa Marehemu tayari umefanyiwa uchunguzi na kukabidhiwa kwa ndugu zake kwa ajili ya taratibu za mazishi.

Kwa upande mwingine Kamanda Hamad ametoa onyo kuelekea siku kuu za pasaka wazazi kutowapeleka watoto kwenye kumbi za vileo na fukwe za Ziwa Tanganyika bila kuwa na uangalizi wa mzazi au Mlezi.

Pia amewataka madereva wa vyombo vya moto wasiendeshe magari kwa mwendokasi huku wakiwa wamelewa kiasi Cha kushindwa kujitambua na kusababisha ajali.

Vile vile wamiliki wa kumbi za starehe wametakiwa kuzingatia usalama katika maeneo yao na kutojaza watu kupita kiasi pamoja na kuzingatia masharti ya leseni zao ambazo zinaonyeaha muda sahihi wa kufunga biashara zao.

Sambamba na hayo Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi limetoa wito kwa Viongozi wa dini kuendelea kukemea maovu kwa waumini kupitia Nyumba za ibada ili kujenga Jamii iliyostaarabika na yenyewe hofu ya Mungu.


Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages