![]() |
| Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Mwanamvua Mrindoko akizungumza na wadau wa mbalimbali wa sekta ya kilimo wakijadili maandalizi ya masoko ya mazao ya kilimo kwa msimu wa mauzo wa mwaka 2022/23 na hali ya utekelezaji wa mpango wa ASDP. |
Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Mwanamvua Mrindoko amewaasa wafanyabiashara kutokupandisha bei za mazao kiholela yanayolimwa na kuvunywa katika mkoa huo.
Maagizo hayo ameyatowa jana katika kikao cha wadau wa kilimo wa Mkoa huo kilichofanyika kwenye ukumbi wa Manispaa ya Mpanda kilichoshirikisha wadau wa sekta ya kilimo na mfugo kwa ajili ya maadalizi ya masoko ya mazao ya kilimo kwa msimu wa mauzo ya mwaka 2022/23 sambamba na utekelezaji wa mpango wa ASDP kwa Mkoa wa Katavi.
Mkuu wa Mkoa huo alieleza kuwa hakuna sababu ya msingi kwa wafanyabiashara kupandisha bei ya mazao ya kilimo hususani ya viazi, mihogo,maragwe,mahidi na mpunga wakati yanazalishwa ndani ya mkoa.

Mrindoko amehimiza kuzingatia utu,kanuni,sheria na taratibu kwa wafanyabiashara kuhakikisha kwamba bei za mazao hayo ambayo kwa kiasi kikubwa ni mazao ya chakula hazipadi kiholela ili kuwafanya wananchi waweze kumudu kununua na kuendelea na ustawi.
“ usalama na uhakika wa chakula ni suala la kiusalama ambalo litapelekea mkoa wetu kuendelea kuwa shwari…kwahiyo upandaji wa bei ya mazao kiholela kutasabisha usalama kuteteleka na sisi kama serikali hatutakubaliana na hilo” alisema Mkuu wa Mkoa Mrindoko
Aidha aliwataka wakuu wa wilaya ya Mpanda,Tanganyika na Mlele kupitia kamati za upangaji bei kuhakikisha wanasimamia ipasavyo ili bei zisipandishwe kiholela na pale watakapoona bei zinapandishwa na hasa kwenye mazao ambayo yanavunywa na kupatikana ndani ya mkoa wa Katavi wachukue hatua kali zinazositahili kwa mujibu wa sheria.
Sambamba na hayo Mkuu wa Mkoa huyo aliwataka wananchi kwenye mavuno wanayovuna kuhakikisha wanawaka akiba ya chakula ya kutosha ili hata likitokea janga la njaa ambao halikutarajiwa basi mkoa wa Katavi usije ukaingia kwenye janga la njaa la wananchi kukosa chakula.

Samweli Mtambalike,Mkuu wa Kituo cha Wakala wa Hifadhi wa Akiba ya chakula Taifa (NRFA) Mkoa amelalamikia ucheleweshwaji wa fedha kwenye taasisi hiyo ambapo fedha hutolewa kwa kuchelewa hali ambayo husababisha wakulima kuanza kuuza mazao yao kwa wafanyabiashara wa kawaida.
Hivyo aliiomba serikali kutoa fedha kwa haraka wakati pale shughuri za uvunaji wa mazao mbalimbali unapofanywa na wakulima,Hali hii itasaidia wakulima kutokomeza mfumuko wa bei kandamizi kwa wakulima.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara na Wamiliki wa Viwanda Vidogo vidogo Mkoa wa Katavi,Shabil Dalla alisema taasisi za kifedha zimekuwa na marshati magumu kwa wakulima katika kuwapatia mikopo kwa ajili ya kujiimarisha kisasa kwenye sekta ya kilimo chenye tija.
![]() |
| Wadau mbalimbali wakiendelea wa sekta ya kilimo wakiendelea kufuatilia mada mbalimbali zilizowasilishwa. |
“ unapofika msimu wa kilimo,mkulima hana fedha za kuwekeza baladala yake anakwenda kukopo kwa watu binafsi kwa dhamana ya kulipa mazao baada ya mavuno kitu ambacho mkulima ameendelea kuwa masikini” Alisema Dalla.
Aliongeza Dalla “…kijana ni mhitimu wa chuo kikuu na anandoto za kujiajili kwenye sekta ya kilimo bahati mbaya anapokwenda kwenye Mabeki kuomba mkopo utashangaa sana Mh Mkuu wa Mkoa anaaza kuombwa hati ya nyumba au kiwanja.Tujiulize kijana huyo alikuwa shule je atapata wapi hizo dhamana”.

