![]() |
| Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mpanda Mh. Haidary Sumry |
Na Walter MguIuchuma,Mpanda
Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi limeviomba vya usalama na ulinzi viwasaidie kuwakamata wadaiwa sungu waliochukua mikopo ya makundi maalumu ya vijana ,wanawake na watu wenye ulemavu ambapo hadi sasa asilimia arobaini ya mikopo iliyotolewa na Manispaa ya Mpanda haija rejeshwa .
Azimio hilo la Baraza la Madiwani lilipitishwa kwenye kikao hicho kufuatia taarifa ya kutoridhisha ya urejeshaji wa mikopo hiyo kwa makundi hayo kwa kipindi cha mwaka huu wa fedha 2021/2022.
Meya wa Manispaa ya Mpanda Haidary Sumry alieleza kuwa hadi sasa ni asilimia 53 tuu ya fedha za mkopo wa makundi maalumu ya vijana,wanawake na watu wenye ulemavu ambazo zimerejeshwa kwa vikundi ambavyo vilipatiwa mikopo huku ikiwa asilimia 43 hawaja rejesha mikopo hiyo .
Alisema wametoa maelekezo kwa Mwanasheria wa Halmashauri ya Manispaa kuangalia vikundi vyote ambavyo havija rejesha mikopo hiyo kwani mikataba yao ya mikopo ipo wazi .
Sumry alisema kuwa kama hawata wachukulia hatua watu hao itaonekana na kwa watu wengine zinatolewa kama ni sadaka jambo ambolo sio kusudio la kutolewa kwa mikopo hiyo ambayo haina tiba.
Hivyo wameviomba vyombo vya Ulinzi na Usalama visaidie kuwakamata watu wote ambao hadi sasa hawajarejesha mikopo hiyo licha ya kuwa wamekuwa wakikumbushwa mara kwa mara lakini wamekuwa hawatekelezi.
Kaimu Mkuu wa Takukuru Wilaya ya Mpanda Ahmed Bukuku alisema kuwa wako tayari kushirikiana na Manispaa hiyo kuwasaka watu wote ambao hawaja rejesha fedha hizo za mikopo za makundi maalumu .
Alisisitiza kuwa kinachotakiwa Takukuru wapewe orodha ya majina hayo ili zoezi hilo la kuwasaka lianze mara moja kwani hiyo itakuwa sio mara yao ya kwanza kufanya kazi kama hiyo ya kuwakata wadaiwa sugu wa fedha za mikopo.
Katika hatua nyingine baraza hilo limempongeza Mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda Sophia Kumbuli kwa kuendesha operesheni ya kukamata watoto wanaozurura mitaani muda wa masomo na kuwachukulia hatua wazazi wa watoto hao na Baraza limeelekeza zoezi hilo liwe endelevu.
