NMB YAZIFUNDA NGO'S KATAVI KUFANYA KAZI KWA UWAZI.

 

Viongozi wa Jukwaa la kuwakomboa Vijana Mkoa wa Katavi wakiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Benki ya NMB

Na George Mwigulu,Katavi. 


Benki ya NMB imeziasa  taasisi zisizo za kiserikali(NGO'S) za Mkoa wa Katavi kuimalisha ufanisi wa utendaji kazi na kufanya kazi kwa haki,uwazi na ukweli hasa kwenye masuala ya mapato na matumizi ya fedha. 

Mwakilishi wa Benki ya NMB Makao Makuu,William Makoresho alitoa wito huo jana kwenye ziara ya kutembelea taasisi kumi zisizo za kiserikili Mikoani Katavi ambapo aliweza kuona namna zinavyo fanya kazi ya kuhudumia jamii kulingana na miongozo yake na kuweza kutoa ushauri kwa taasisi hizo. 

Makoresho akizungumza katika Ofisi ya Taasisi ya Youth Redemption Organization iliyopo Manispaa ya Mpanda alisema kuwa Taasisi nyingi zimekuwa zikianzishwa kwa malengo mazuri ya kuhudumia jamii lakini baadhi yake zimekuwa dumavu na kufa.

Sababu ya kutokufanikiwa kiutendaji na kufa kwa baadhi ya taasisi nyingi zisizo za kiserikali ni kutokana na uendeshaji wake kugubikwa na msingi ya kutokuwa na uwazi kwa viongozi wa Taasisi hizo hasa kwenye nyanja za kifedha na kusababisha kutokuaminiana miongoni mwao.

Mwakilishi huyo wa Benki ya NMB  aliweka wazi kuwa kama Taasisi zitazingatia malengo ya kiutendaji kwa kufanya kazi mahususi za  mwelekeo halisi wa maana na nia za kuanzishwa kwa taasisi hizo ambazo ni uwazi na ukweli zitaweza kupiga hatua kubwa za kuinufaisha jamii na taifa kwa ujumla na sio kwa kuendekeza migogoro itokanayo na kukosekana kwa uwazi na ukweli.


Viongozi wa Jukwaa la kuwakomboa vijana Mkoa wa katavi wakiwa na Viongozi wa Benki ya NMB katika mazungumzo juu ya namna Bora ya kufanya Kazi na jamii.


"... kama NGO's mnapaswa kufanya kazi kwa mujibu wa sheria na kwa kufuata miongozo mliyopatiwa na Serikali ili kuepuka kuwa daraja la kujipatia fedha kwa mgongo wa kuisadia jamii" alisema Mwakilishi huyo wa Benk ya NMB.

Vilevile alifafanua kuwa jamii inakabiliwa na changamoto nyingi huku taasisi zisizo za kiserikali zinabeba wajibu mkubwa wa kuzifikia ili kuisaidia serikali kwenye utendaji kazi. 

Aidha alisema kuwa Benk ya NMB iko tayari kushirikiana na taasisi hizo kwa ajili ya kufungua fursa zaidi wezeshi za kiutendaji ambapo aliwaomba pia kufanya ushirikiano na Taasisi nyingine kubwa kama vile Amref,Mkapa Foundation na vyinginezo ikiwa ni mkakati wa kuongeza uwanda mpana wa kuifikia jamii husika. 

Meneja wa Benk ya NMB Mkoa wa Katavi,Hygrace Mwanjuguja licha ya kuipongeza taasisi ya Youth Redemtion Organization ya Manispaa ya Mpanda kwa kazi nzuri iliyojiwekea kufanya alisema kuwa kuanzishwa kwake iwe chachu ya kusaidia kulifikia kundi la vijana na kama Benki ya NMB wako tayari kutoa mafunzo ya matumizi sahihi ya fedha na kutoa fursa za mikopo ambayo hutolewa kwa  vijana. 

Mwanjuguja alisema Benki ya NMB hawatasita kushirikiana na Youth Redemption Organization ili kuwaonesha vijana fursa zinazopatikana katika Mkoa wa katavi kwenye sekta za kilimo,ufugaji na zingine nyingi.

Mkurugenzi wa Youth Redemption Organization,Saimoni John aliishukuru Benki ya NMB kwa kuwapatia mawazo yenye lengo la kuzijenga taasisi za mkoa wa Katavi kwa misingi ya kufuata kanuni na taratibu za nchi Ili kuwatumikia vijana na kuwakomboa kwenye nyanja za afya,uchumi na zingine nyingi. 

John aliziomba na Taasisi nyingine kubwa  na mabenki mbalimbali kuiga mfano wa benki ya NMB kwa ajili ya kujitoa kwa Taasisi zilizopo Mikoani ili kuzijengea uwezo wa kujiendesha kiutendaji. 

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages