Na Walter Mguluchuma .
Katavi.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi linawashikilia watu kumi na moja wakiwa na vitu mbalimbali vya wizi vilivyo ibiwa kwenye nyumba za watu zikiwemo TV,Magodoro Mafuta ya Diseli na Pikipiki iliyoibiwa Mkoani Kigoma .
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi Ali Makame Hamad amesema watuhumiwa hao wamekamatwa kufutia msoko mkali uliofanywa na Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na wananchi waliotoa ushirikiano kwa Jeshi la polisi .
Alisema mnamo Aprili 29,2022 Jeshi la Polisi lilimkamata mtuhumiwa Hadija Ibrahimu (24) Mkazi wa Mtaa wa Nsemlwa akiwa na TV moja aina ya Singsung Flatscreen nchi 21 mali inayodhani kuwa ni ya wizi pia alikamatwa Christina Yahaya (41) mkazi wa Mtaa wa Mnazi mmoja akiwa na godoro moja 5 kwa 6 mali inayodhani kuwa ya wizi .
![]() |
Aidhaalikamatwa mtuhumiwa Ramadhani Idd akiwa na godoro moja 5 kwa 6,radio moja aina ya Sipiano na speker zake mbili vilevile alikamatwa mtuhumiwa Daud mkazi wa Mtaa wa Nsemlwa akiwa na begi mbili za nguo ,zulia moja na vyombo mbalimbali vya ndani . |
Kamanda Ali Makame Hamad alieleza kuwa kwenye msako huu wamefanikiwa pia kumkamata mtuhumiwa Joseph Makame (30) Mkazi wa Mtaa wa Makanyagio akiwa na pikipiki aina ya Kinglion yenye Namba za usajiri MC.755 DCL ambayo iliibiwa Mkoani Kigoma .
Pia katika msako huo wamefanikiwa kukamata Tv moja aina ya LG inchi 32,tv moja aina ya Home base nchi 50,magodoro matatu,friji moja,radio tatu pamoja na subwoofa aina ya aborder.
Alisema watuhumiwa hao 11 waliokamatwa bado wanaendelea kushikiliwa na jeshi la polisi pamoja na walioshirikiana nao kufanya uhalifu wa kuvunja na kuiba vitu hivyo ili kuweza kupata mtandao wote na mara uchunguzi utakapo kamilika watuhumiwa watafikishwa Mahakamani.
Katika tukio jingine huko katika Kijiji cha Ilalangulu Kata ya Kibaoni Wilaya ya Mlele Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi limewakamata watuhumiwa wanne wakiwa na mafuta ya dizeli lita 200 yakiwa yamehifadhiwa kwenye madumu ya lita ishirini.
Mafuta hayo wameyaiba kwenye Kampuni ya Ujenzi Morden Agro Ltd inayofanya kazi ya ujenzi wa barabara kutoka Kibaoni kwenda Sitalike ambao watuhumiwa hao ni wafanyakazi wa kampuni hiyo.

