![]() |
| Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi ACP Ali Makame Hamad |
Na Walter MguIuchuma
Katavi
Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi katika kuhakikisha sikuuu ya Eid el Fitri inasherekewa kwa amani katika Mkoa huo limejipanga kuimarisha ulinzi kwenye maeneo yote na kwenye maeneo ya nyumba za Ibada pamoja na barabara zinazoingia na kutoka nje ya Mkoa wa Katavi .
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Ali Makame Hamad amewaambia Waandishi wa Habari kuwa kama ambavyo watu wanafahamu kuwa waumini wa dini ya Kiislamu wapo katika mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani .
Hivyo katika kuisherekea sikukuu hiyo kutafanyika ibada kwenye maeneo mbambali ya Mkoa wa Katavi na moja ya jukumu la Jeshi la Polisi ni kuhakikisha waumini wanafanya ibada kwa amani na utulivu mkubwa .
Kamanda Ali Makame Hamad alisema katika kuhakikisha sikukuu hiyo inasherekewa kwa amani na utulivu Jeshi la Polisi mkoani hapo limejipanga vyema kuimarisha ulinzi kwenye maeneo yote hususani nyumba za Ibada .
Amebainisha kuwa kutakuwa na doria za muda wote ambapo Askari watakuwa katika doria za miguu ,pikipiki pamoja na magari kwenye maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Katavi.
Amewashukuru wananchi wa Mkoa wa Katavi kwa ushirikiano wanaendelea kuutoa kwa Jeshi la polisi kwa kutowa taarifa mbalimbali za uhalifu na kuweza kusaidia wahalifu kukamatwa kabla ya kufanya uhalifu au baada ya kufanya matukio .
Alisema hali hiyo ya Ushirikiano baina ya Polisi na Wananchi imepelekea Mkoa wa Katavi kuwa shwari kipindi chote cha mwaka huu kuanzia Mwezi Januari hadi sasa.
