MGANGA WA KIENYEJI MBARONI KWA KULAWITI WATOTO 6 WAKATI AKIWAPATIA MATIBABU

Kaimu Kamanda wa Polisi  Mkoa wa Katavi  Sylivester Ibrahim akitoa  taarifa kwa Waandishi wa  Habari juu ya kukamatwa kwa mganga wa  kienyeji  kwa tuhuma za kuwalawiti watoto sita wakati akiwapatia tiba ya asili.


Na  Walter Mguluchuma

   Katavi .

Jeshi la Polisi  Mkoa wa Katavi linamshikilia mganga wa kienyeji Akili  Abakuki ( JIMMY) (38)  Mkazi wa Majengo Manispaa ya Mpanda kwa tuhuma za kuwalawiti watoto sita mida ya usiku wakati alipokuwa  akiwapatia matibabu ya  tiba za asili.

Kaimu  Kamanda wa Jeshi la Polisi wa Mkoa wa Katavi  Sylivester  Ibrahim amesema mtuhumiwa huyo alikamatwa Mei 8 majira ya saa saba  mchana  katika eneo  la Hospitali ya Mkoa wa Katavi  iliyoko katika Kata ya Kawajense Manispaa ya Mpanda .

Amesema mtuhumiwa  huyo alikamatwa baada ya   mama mmoja mkazi wa Mtaa wa Makanyagio alipogundua mtoto wake  wa miaka 10 mwanafunzi wa darasa la tatu jina limehifadhiwa  aliyekuwa amempeleka kwa mganga huyo kupatiwa matibabu ya uganga wa kienyeji kuwa amelawatiwa.

Kaimu  Kamanda wa Polisi   alisema baada ya kupatikana taarifa hizo Jeshi la Polisi lilifanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo ambae pia alikuwa amewalawiti watoto wengine watano wakati akiwafanyia matibabu ya  tiba  za  kienyeji wenye umri kati ya  miaka 6 na  miaka 12.

Amebainisha kuwa  wazazi wa watoto hao walikuwa wakiwapeleka  watoto wao  kwa mganga  huyo  kwa ajili ya  kupatiwa tiba  za kienyeji  ambapo  katika tiba  hizo  Mganga huyo  alikuwa akitowa masharti  kuwa tiba zake ni lazima azitowe  usiku   hivyo ni lazima watoto hao walale kwake  bila wazazi wao kuwepo  .

 Ilipokuwa ikifikia  usiku  mganga  huyo alikuwa  anawadanganya  kwa kuwapatia  zawadi  ndogo ndogo  kama  pipi,biskuti na jojo  na kisha anawavua nguo  na kuwapaka mafuta mwili mzima  na kuwalawiti .

Kaimu  Kamanda   Sylivester  Ibrahim alisema vitendo hivyo  vya kuwalawiti  watoto hao alikuwa  akivifanya  ndani ya chumba chake alichokuwa akiishi usiku wa manane  huku akiwatishia watoto hao wasiwaambie wazazi wao kama amewafanyia kitendo hicho .

Aidha  Kaimu Kamanda amewahimiza  wazazi Mkoani Katavi kufatilia   vitendo ambavyo wanaweza kuwa wamefanyiwa watoto wao  na pia wazazi waache tabia ya kuamini Imani potofu  na  za kishirikina. 

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages