![]() |
| Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi Sylivester Ibrahim |
Na Walter Mguluchuma
Katavi .
Watu wanne wanashikiliwa na Polisi Mkoa wa Katavi kwa tuhuma za kuwakamata na kilo 600 za nyama ya kiboko huku wakiwa na bunduki aina ya Rifle inayomilikiwa na Halmashauri ya Nsimbo .
Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi wa Mkoa wa Katavi amewataja watuhumiwa hao waliokamatwa na nyama ya kiboko kuwa ni Gilberti Kaswiza (45) Mkazi wa Ilembo Manispaa ya Mpanda ambae alikuwa na wenzake Wenseslaus Wiliam (KARUMENDO)ambaye ni Askari wa Idara ya wanyamapori Halmashauri ya Nsimbo,Ally Juma(41),Mashaka Khamisi (40) pamoja na Kasala Issa(42) wote wakazi wa Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi.
Alisema watuhumiwa hao walikamatwa Mei8,2022 majira ya saa tisa na nusu mchana katika Kijiji cha Tulieni Kata ya Itenka Wilaya ya Mpanda wakiwa wamepakia nyama hiyo ya kiboko kilo 600 kwenye gari yenye Namba za usajiri T 905 BTM inayomilikiwa na Joseph Misasi Fundi magari mkazi wa Mtaa wa Nyerere Manispaa ya Mpanda .
Watuhumiwa hao walimuuwa kiboko huyo kwa kutumia silaha aina ya Rifle yenye Namba za usajiri G.4687 ambayo inamilikiwa na Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo .
Amebainisha kuwa kukamatwa kwa watuhumiwa hao kulifuatia taarifa zilizofikishwa Hifadhi ya Taifa ya Katavi ya kuuwawa kwa mnyama huyo na ndipo walipoanza msako na kuwakamata watuhumiwa hao wakiwa na nyama hiyo.
Watuhumiwa hao wanatarajiwa kufikishwa Mahakamani kujibu tuhuma zinazo wakabili juu ya tukio hilo la kukutwa na nyara za serikali.
