NMB YAPIGA TAFU WIKI YA UHAMASISHAJI UNYWAJI MAZIWA KITAIFA MKOANI KATAVI

Katibu Tawala Mkoa wa Katavi Rodrick Mpogolo(katikati) akiipongeza Benki ya NMB kwa kuwa  Mdhamini wa Maadhimisho wiki ya unywaji Maziwa inayofanyika Kitaifa Mkoa wa Katavi.(Picha na Walter Mguluchuma)

Na  Walter  Mguluchuma

   Katavi

Benki ya Nmb imekuwa mdau mkubwa kwa Serikali,Sekta ya Kilimo ,Uvuvi na mifugo pia wadhamini wa Maadhimisho wiki ya unywaji maziwa Kitaifa inayoadhimishwa Mkoani Katavi  mwaka 2022.

Nmb imekuwa ni sehemu ya Maendeleo ya kilimo kwa upande wa uwezeshaji na  wamekopesha fedha nyingi kwenye Sekta hiyo ya Kilimo na Uvuvi pamoja na uzalishaji wa maziwa na ufugaji wa Ng’ombe.

Hayo yamesemwa na Mwakilishi wa Meneja wa Benki ya NMB  Kanda ya Magharibi Berdon Mwakatobe wakati akikabidhi T-sheti 300 zilizizotolewa na Benki hiyo kwa Katibu Tawala Mkoa wa Katavi aliepokea kwa niaba ya Waziri wa Mifugo zitakazo tumika kwenye Maadhimisho wiki ya unywaji maziwa  Kitaifa yanayofanyika Mkoani Katavi.

Mwakilishi wa Meneja wa Benki ya  NMB Kanda ya Magharibi Berdon Mwakatobe akikabidhi  T-shirt 300 kwa Katibu Tawala Mkoa wa Katavi Rodrick Mpogolo kwaajili ya Maadhimisho ya Wiki ya uhamasishaji unywaji  Maziwa inayofanyika Kitaifa Mkoa wa Katavi ikiwa ni sehemu ya udhamini wa maadhimisho hayo uliotolewa na Benki hiyo ya NMB.

Mwakatobe ameeleza kuwa licha ya  Benki hiyo ya NMB kudhamini maazimisho hayo ya wiki ya unywaji maziwa wamekuwa wadau wakubwa wa Maendeleo kuliko benki yeyote hapa nchini kwa kukopesha fedha nyingi katika sekta za Kilimo,Mifugo, Uvuvi na Sekta ya uzalishaji wa  Maziwa kwa lengo la kuisadia Serikali katika kumkomboa mwanachi kiuchumi.

Amebainisha kuwa Benki hiyo imetoa shilingi Bilioni 100 ambazo zimekopeshwa kwa asilimia10 na zimekwisha na wameongeza fedha nyingine ambazo kwa sasa zinakopeshwa kwa asilimia 9 na zipo hivyo wadau wote wa kilimo wanakaribishwa kujitokeze kukopa kwa maendeleo yao na Taifa kwa ujumla.

Aidha alisema kuwa NMB wanaendelea kuboresha sekta mbalimbali ikiwemo Umwagiliaji,Tumbaku na sekta nyingine zote za kilimo na katika Maadhimisho ya wiki ya unywaji maziwa  NMB watatoa huduma mbalimbali kwa wateja wao ikiwemo kufungua Akaunti kutoa elimu ya mikopo ya NMB kwa ajili ya Wajasiriamali.

Katibu Tawala  Mkoa wa Katavi Rodrick Mpogolo aliishukuru NMB na Bodi ya Maziwa kwa kuleta Wiki  ya uhamasishaji unywaji wa maziwa Kitaifa katika Mkoa wa Katavi.

Alisema Mkoa wa Katavi ni miongoni mwa Mikoa mitano yenye Idadi kubwa ya mifugo katika taifa letu la Tanzania.

"......Mkoa wa Katavi unamaziwa mengi sana lakini inawezekana uhamasishaji wa unywaji  maziwa bado upo chini na wengi wetu hatunywi maziwa bila kujua kwamba maziwa ni lishe inayoboresha afya zetu na ukinywa maziwa umepata mlokamili"alifafanua Mpogolo

Alisema pia bodi ya Maziwa na NMB wameleta kitu muhimu sana kwa wanachi wa Mkoa wa Katavi kwa ajili ya Maendeleo na Ustawi wa Kiuchumi na Afya.

Amesisitiza kuwa kazi ya uhamasishaji unywaji wa maziwa katika Mkoa wa Katavi bado nikubwa kwani kuna baadhi ya familia zinakunywa maziwa mara moja  kwa mwezi hivyo uhamasishaji kwa wadau bado unahitajika.

Nae Mwakilishi wa Msajili wa Bodi ya Maziwa Tanzania Christerbel Swai aliishukuru NMB kwakuwa wadau muhimu katika shughuli muhimu kwenye nchi yetu ya Tanzania ya uhamasishaji unywaji wa maziwa.

Swai alisema shughuli ya uhamasishaji unywaji wa maziwa hapa nchini hufanyika kila mwaka Mwezi wa Sita kwenye shughuli hizi wadau wa maziwa huwa wadhamini wakuu wa shuguli hizi na mwaka huu Benki ya NMB imewadhamini jumla ya Tisheti 300.

Katibu Tawala Mkoa wa Katavi Rodrick Mpogolo akimkabidhi Mwakilishi wa Msajili wa Bodi ya Maziwa Tanzania Christerber Swai T-shirt 300 zilizotolewa na Benki ya NMB kwa ajili ya Maadhimisho ya wiki ya uhamasishaji unywaji Maziwa inayofanyika Kitaifa Mkoa wa Katavi(Picha na Walter MguIuchuma)


Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages