WAFANYABIASHARA KATAVI WALIA NA TANESCO KUKATIKA KWA UMEME MARA KWA MARA.

 

William Mbogo,Mfanyabiashara na Diwani wa kata ya Majengo Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi


Na   Paul  Mathias

Wafanyabiashara na wamiliki wa viwanda Mkoa wa Katavi wamelalamikia kukatika kwa umeme  mara kwa mara kumekuwa kukiathili shughuli za uzalishaji mali kutokana na huduma hiyo kuwa ya kususua na kuufanya Mkoa wa Katavi kuwa hatarini kukosa wawekezaji.

Malalamiko hayo ya  watumiaji wa umeme Mkoa wa katavi wameyatowa  kwenye kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa Katavi Resort baina yao  na Viongozi wa  Shirika  la Umeme (TANESCO) Mkoa wa katavi .

Miongoni mwa Wamiliki hao akiwepo Shabil  Dalla  Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara wa Viwanda na Wakulima Mkoa wa Katavi (TCCIA)ametishia kufunga kiwanda cha kuchakata kokoto kwa kuwa huduma hiyo imekuwa haipo katika uhalisia wake kutokana  na  kukatika katika   kwa umeme  mara kwa mara.

Dalla alisema wafanyabiashara  hawaridhishwi na huduma  ya umeme  kutokana na kazi wanazozifanya kutegemea umeme muda wote hivyo mara huduma hiyo inapokosekana imekuwa  ikisababisha  gharama za uendeshaji kuwa kubwa.

Aliongeza kuwa Mkoa upo hatarini kupoteza wawekezaji kwakuwa hakuna huduma ya uhakika ya umeme kwa wamiliki wa viwanda hivyo inakuwa vigumu wawekezaji kuja kuwekeza  Mkoani  Katavi.

".....Mh Meneja wa Tanesco mimi nikuombe sana tena sana sana nitakuwa mpiga kelele wa kila siku sijalizika na hali ya umeme na ninawaambia wafanya biashara wenzangu wanaotaka kuja kuwekeza  Katavi  kuwa  huduma za umeme bado hazilishi"alisema Dalla

Nae William Mbogo mmoja wa watumiaji wa umeme kwenye kiwanda  chakuchakata kokoto amebainisha kuwa kumekuwa na ongezeko kubwa la uhitaji wa umeme katika Mkoa wa Katavi kupitia Miradi ya REA lakini kitengo cha mafundi Tanesco Katavi nacho lazima kiendane na uhalisia wa ongezeko hilo kwa kuwa kinaonekana kuzidiwa kwakuwa unaweza kutoa taarifa ya tatizo na ikachukua muda mrefu kufika kwenye tatizo.

Mbogo alisema kuwa suluhisho la tatizo la kukatika kwa umeme huenda ikawa kuunganishwa katika Grade ya Taifa kama Serikali ambavyo imekuwa ikisema mara mara pia ametoa  ushauri kwa Viongozi wa Tanesco Mkoa wa Katavi kuwatumia Wabunge wa Mkoa wa Katavi waliopo kwenye maeneo yao kwaajili ya kuongeza nguvu katika kuyafikisha matatizo hayo kwa Waziri kwa kuwa wao wanawajibika kwa wananchi.

"Nilikuwa na ushauri mmoja maeneo mengine ninyi Tanesco inaweza kuwa hamuwezi  labda Wizara,mimi niwashauri tu tumieni wabunge wabunge wananguvu hasa katika kipindi hiki cha bajeti"alibainisha Mbogo``

Kwa upande wake Sambo Luhende akichangia hoja ya kukatika kwa umeme kwenye maeneo ya viwanda vya kuchakata nafaka alisema hajui kama ipo sheria ya kuwataarifu wateja kabla ya kukatika kwa umeme lakini hilo limekuwa ni changamoto kubwa wakati mwingine hukaa siku tatu bila umeme hali hii hutishia uendeshaji wa viwanda.

Anasema kuwa ``Tumejaribu kuwasilisha matatizo yetu kwa Meneja mara kwa mara shida nini tupewe uhakika wa umeme shida nini"alisisitiza Luhende

Aidha katika hatua nyingine Leonard Lusaganya Mwakilishi wa Flamingo Foods Company Limited kutoka kiwanda cha kuchakata Mazao ya nafaka Majimoto Halmashauri ya Mpimbwe Wilaya ya Mlele alieleza kuwa inawawia vigumu kusafirisha nafaka kutokana na kukatika katika kwa umeme kwa kuhofia kukosa wateja kwa kuwa umeme sio wa uhakika hawajuwi muda ambao huwa unakuwepo.

Akijibu hoja mbalimbali za Watumiaji wa Umeme katika Mkoa wa Katavi Kaimu Meneja wa Shirika la Umeme Tanesco  Mkoa wa Katavi Mhandisi  Godfrey Josephat amesema kuwa kuna idadi kubwa ya wamiliki wa viwanda wanaotaka kuunganishiwa huduma ya umeme lakini wanashidwa kufanya hivyo kwakuwa umeme uliopo ni mdogo.

Kaimu Meneja Tanesco Mhandisi Godfrey Josephat


Alieleza kuwa kwa uhalisia hali ya uzalishaji wa umeme na mahitaji ya wananchi bado ni changamoto kubwa ndiyo maana Serikali imeanza kutekeleza Mradi wa grade ya Taifa kutoka Mkoa wa Tabora na kuwaomba wateja hao kuendelea kuwa wavumilivu na kuipokea huduma iliyopo wakati mipango ya kuimarisha huduma hiyo katika Mkoa wa Katavi ikiwa inaendelea

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages