Na Walter Mguluchuma
Katavi .
Benki ya MNB imetoa mkopo kwa waendesha Bajaji na Boda boda wa Mkoa wa Katavi wenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 81 ikiwa ni jitihada za kuiunga Mkono Serikali kupunguza tatizo la ajira kwa vijana waweze kujikomboa kiuchumi na kupunguza vijana wasio na ajira hapa nchini .
Benki hiyo ya NMB imekabidhi mkopo huu kwenye hafla iliyofanyika katika eneo la Benki ya NMB tawi la Mpanda na Mgeni Maalum Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko alikabidhiwa mkopo huo wa bajaji na pikipiki kwa walengwa.
Akizunngumza kwenye hafla hiyo Meneja mauzo wa NMB Kanda ya Mgharibi Trifon Melkiory alisema kuwa Benki ya NMB imeanzisha mpango wa kuwakopesha waendesha bajaji na piki piki kupitia mpango unaoitwa MASTABODA .
Amebainisha kuwa mpango huo wa MASTABODA utawanufaisha vijana wengi kiuchumi hapa nchini na kuwasaidia vijana wengine kujiari kwani kundi hilo lina Idadi kubwa ya watu.
Melkiory amesema wametowa mkopo wa bajaji nane na pikipiki tatu zenye thamani ya shilingi Milioni 81,609,000,000 kwa ajili waendesha bajaji na boda boda wa Mkoa wa Katavi waliokidhi vigezo vya kukopeshwa na Benki hiyo ya NMB.
Amefafanua kuwa Mkoa wa Katavi umekuwa wa kwanza kukopesha kiwango kikubwa cha fedha ukifuatiwa na Mkoa wa Tabora ambao wamekopeshwa hadi sasa jumla ya bajaji sita.
Nae Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph amesema kuwa NMB kwa kutowa mkopo huu wameiunga mkono Serikali na wamepunguza tatizo la ajira hivyo ni vema vijana waitumie fursa hiyo waliyopewa vizuri.
Mkuu wa Mkoa Katavi Mwanamvua Mrindoko kwa upande wake aliwataka wananchi wa Mkoa wa Katavi kuhakikisha wanachangamkia fursa zinazo tolewa na benki ya NMB kwa kujipatia mikopo ili kuweza kukuza uchumi wao na wa Mkoa wa Katavi na nchi kwa ujumla .
Aliwasisitiza vijana hao kuhakikisha wanakuwa na nidhamu katika kurejesha mikopo hiyo ya bajaji na boda boda kwa kuzingatia masharti ya mikopo ya Benki ya NMB ili benki hiyo iendelee kuwaamini na wengine waweze kunufaika na mpango huu wa MASTABODA .
Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Haidary Sumry alisema kuwa amefarijika sana kwa NMB kutoa mkopo huo kwani utasaidia hata mapato ya Manispaa ya Mpanda kuongezeka hivyo aliomba benki hiyo itowe tena mikopo hiyo na kwa vijana wengine .
Kwa upande wake Mlezi wa waendesha Bajaji na Boda boda Mkoa wa Katavi Beda Katani alisema kuwa vijana wa Mkoa wa Katavi wamepata fursa kubwa kutoka Benki ya NMB kuliko Mikoa mingine hivyo waitumie vizuri fursa hiyo .
![]() |
| Tawi la Benki ya NMB Mpanda lililopo eneo la madukani Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi. |

