NA
Walter Mguluchuma,Katavi.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Katavi Ali Hamad Makame amewaambia Waandishi wa Habari
kuwa tukio hilo la kinyama limetokea hivi karibuni katika Kijiji cha Kagunga
Wilayani Tanganyika .
Mtuhumiwa Jackson siku hiyo ya tukio alimvizia mtoto huyo jina limehifadhiwa wakati akitoka nyumbani kwao kwenda nyumba ya jirani kwa lengo la kucheza na watoto wenzake.
Amesema Kamanda ndipo mtuhumiwa alipomkamata na kumvutia kichakani kisha alimvua nguo zake alizokuwa amevaa na kuanza kumbaka na kumlawiti huku akiwa amemkaba shingoni na kumwamuru mtoto huyo asipige kelele za kuomba msaada
Kamanda Ali Makame alisema baada ya mtuhumiwa kukamatwa na Jeshi la Polisi uchunguzi wa awali umebaini kuwa tukio hilo linahusiana na imani za kishirikina kwani mtuhumiwa alikuwa amehaidiwa kulipwa ng'ombe watatu baada ya kutekeleza kitendo hicho.
Alieleza kuwa mtuhumiwa baada ya kutenda kitendo hicho alitakiwa na mtu huyo aliyemtuma kutekeleza tukio hilo aende akamwonyeshe shambani kwake ili iwe zindiko kwa ajili ya shamba lake lisiwe linaibiwa mazao .
Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi linaiasa jamii na kukemea vikali matukio ya namna hii na halita sita kumchukulia hatua mtu yeyote atakaebainika kujihusisha na matendo ya namna hiyo.
Kamanda
Makame amesema Jeshi la polisi wanaendelea na upelelezi wa tukio
hili na pindi upelelezi utakapo kamilika mtuhumiwa atafikishwa
Mahakamani mara moja.