DC JAMILA AHIMIZA UZALENDO ZOEZI LA SENSA.

  

Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph akiwahutubia wahitimu wa mafunzo ya Sensa ya watu na makazi kwa niamba ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko.

Na Mwandishi Wetu,KTPC Katavi.

Wahitimu wa mafunzo ya Sensa ya Watu na Makazi katika mkoa wa Katavi wameaswa kuzingatia uzalendo na weredi kwenye kuwafundisha makalani na wasimamizi wa Sensa ngazi ya wilaya mkoani hapo.

Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya Sensa ya watu na makazi yaliyofanyika kwa siku 21 katika ukumbi wa idara ya maji Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi,

Wahitimu wa mafunzo ya Sensa ya Watu na Makazi katika mkoa wa Katavi wameaswa kuzingatia uzalendo na weredi kwenye kuwafundisha makalani na wasimamizi wa Sensa ngazi ya wilaya mkoani hapo.

 Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph akizungumza kwa niamba ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi  Mwanamvua Mrindoko kwenye kufunga mafunzo ya siku 21 ya wakufuzi wa sensa  yaliyofanyika ukumbi wa idara ya Maji Manispaa ya Mpanda alieleza kuwa kutamatika kwa mafunzo hayo ndiyo mwanzo wa kwenda kufanya kazi kwa uadilifu katika maeneo waliyopangiwa.

 Jamila alieza kuwa suala la uandilifu ni muhimu kwenye utekelezaji wa kazi  ya sensa  hasa watakapokuwa kwenye vituo vyao vya kazi ambako wataedesha mafunzo kwa wasimamazi na makalani wa sensa hivyo wanapaswa kuwa mfano mzuri kwao.

 “ mkifanya kwa weredi,uadilifu na kujituma huo utakuwa ni uzalendo mkubwa kwa nchi kwa sababu mtaisaidia serikali kupata takwimu sahihi  ambazo zitafanikisha kupanga utoaji wa huduma mbalimbali kwa wananchi hasa za maendeleo” alisema Mkuu wa Wilaya.

Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya Sensa ya watu na makazi yaliyofanyika kwa siku 21 katika ukumbi wa idara ya maji Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi,

Mkuu wa wilaya huyo alisema “ wahitimu nafahamu mmejifunza namna ya kuuliza maswali pamoja na madodoso ambayo yatawasaidia kwenye kuuliza maswali ikiwa ni sehemu ya kupata taarifa muhimu pamoja na  mafunzo hayo yamewapatia nyenzo muhimu na kilichobaki nikwenda kuwajibika ipasavyo kwa kuwa watendaji wazuri kwa kuwasimamia Makalani na wasimamizi wa sensa ngazi ya wilaya.

 Joyce Msoka,Mkufunzi kiongozi wa Sensa ya Watu na Makazi alisema kuwa mkoa wa Katavi unachangamoto ya upatikaji  wa idadi ya watu kutokana na hali ya watu wake kuwa na mwingiliano wa kuingia na kutoka unaosababishwa na ukuaji wa sekta ya kilimo na madini.

 Mkufunzi huyo alisema kuwa hali hiyo itaifanya kazi ya kuhesabu watu kuwa na ugumu,hivyo makalani na wasimamizi wa maudhui wanapaswa kuwa wavumilivu kwa kufanya kazi kwa moyo wa kizalendo kwa nchi yao.

Joyce Msoka,Mkufuzi kiongozi wa mafunzo ya Sensa ya Watu na Makazi ya siku 21 yaliyofanyika Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi akitoa neno kwa washiriki wa mafunzo waliohitimu.

 “ suala muhimu hapa ni kupata taarifa sahihi ambayo itakuwa ni silaha kwenye kufanikisha zoezi la sensa  kwa ajili ya usitawi wa jamii” alisema Joyce.

Nao baadhi ya Wahitimu walioshiriki kwenye mafunzo hayo ya siku 21, Mariamu Yasini ameeleza kuwa Mafunzo hayo yamekuwa chachu kwake kwani atakwenda kukisimamia kile alichofundishwa na wakufuzi  ngazi ya mkoa.

 Mariamu ameeleza kuwa yale yote yaliyo zungumnzwa na Wakufunzi wakuu wataenda kuyaenzi kazi kwa vitendo na wapo tayari katika kuchapa kazi hiyo kwa masilahi mapana ya Mkoa na Taifa kwa ujumla.

 Zoezi la sensa ya watu na Makazi hapa nchini linatalajia kufanyika Mnamo Agust 23 mwaka huu nchi nzima huku sense hiyo ikitajwa kuwa ya Sita Tangu Tanzania kupata uhuru na sense ya mwisho ilifanyika hapa nchini mwaka 2012.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages