Baadhi ya watoto na walimu wa YUMA PRE AND PRIMARY SCHOOL wakifurahi kwa pamoja kwenye shule hiyo mara baada ya masomo. |
Wananchi wa Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wamefurahia kuanzishwa kwa shule mpya ya kisasa ya YUMA PRE AND PRIMARY SCHOOL iliko katikati ya Mji wa Manispaa ya Mpanda .
Baadhi ya wakazi wa Manispaa hiyo wamesema wamevutiwa sana na miundo mbinu ya shule hiyo inayofundisha wanafunzi kwa masomo ya mchepuo wa masomo ya lugha ya kingereza kuanzia darasa la awali .
Salome
Mwanandeje Mkazi wa Mtaa wa Kawajense
ambae ni mzazi wa mwanafunzi anae
soma kwenye shule hiyo inayofundisha masomo ya mchepuo wa kiingereza ameeleza kuwa
shule hiyo ni mkombozi katika
kuinua swala zima la elimu katika Mkoa wa Katavi na nchi
kwa ujumla.
Amebainisha kuwa imekuwa ni nadra kuona shule kama hizo zikianzishwa zikiwa na mazingira mazuri ya watoto kujifunzia na kupata elimu bora kwa watoto.