Na Paul Mathia
Katavi
Waandishi
wa Habari katika Mkoa wa Katavi wameaswa kuendelea kuuhabarisha wa Mkoa wa
Katavi kwa Mambo yanayofanywa na serikali katika sekta Mbalimbali ili wananchi
wafahamu namna serikali inanyo sogeza huduma hizo kwa Wananchi.
Waandishi wa Habari katika Mkoa wa Katavi wameaswa kuendelea kuuhabarisha wa Mkoa wa Katavi kwa Mambo yanayofanywa na serikali katika sekta Mbalimbali ili wananchi wafahamu namna serikali inanyo sogeza huduma hizo kwa Wananchi.
Kauli hiyo imetolewa na Deodatus Kangu Afisa utumishi wa Manispaa ya Mpanda aliye Mwakilisha Msitahiki meya wa Manispaa ya Mpanda Haidary Sumry kwenye Maadhimisho ya uhuru wa vyombo vya habari yaliyofanyika katika ukumbi wa Katavi Resort Mpanda Mjini.Kangu
amesema kuwa Waandishi wa Habari ni vipasa sauti kwa umma kwa kuwafikia
wananchi kwa ukubwa nakwa haraka zaidi kwa kuandika na kutangaza Mambo
mbalimbali ambayo yamekuwa yakifanywa na serikali.
‘’nitoe
shukurani sana kwenu waandishi wa Habari mmekuwa Vipasa sauti vya kuwafikia wananchi
kwa ukubwa kwa mambo mengi sana ambayo serikali imekuwa ikiyafanya kwani siyo
kila mmoja anaweza akayaona lakini huwatunaamini kwamba tukiwashirisha masuala
yote hayo yanawafikia wananchi’’ amesema Kangu.
Amesema
kazi ya uandishi wa habari huleta usitawi wa Jamii kupitia Habari zinazoandikwa
na kuleta Mtizamo chanya kwenye Jamii ili kuongeza uwajibikaji kwa Mamlaka
zilizopo ili wananchi waweze kupata huduma mbalimbali.
Mwenyekiti
wa Klabu ya wandishi wa habari mkoa wa Katavi walter Mguluchuma amewaasa
waandishi wa habari kufanya kazi zao kwa kuzingatia miiko ya uandishi wa habari
Kwa
upande wake Rais wa Umoja wa Klabu za waandishi wa habari Tanzania Deogratius Nsokolo
amesema kuwa anaishuru serikali ya awamu ya Sita kwa kukubali kuanza mchakato
wa Ulekebishaji wa sheria za habari ambazo zilikuwa zinaoneka kuwa kandamizi
kwa waanndishi wa habari hapa nchini.
Nsonkolo
amewakumbusha waandishi wa Habari kuendelea kuwa sauti ya watu wasio kuwa na
sauti kwa kuibua changamoto zao ili serikali iweze kuwajibika kwa kupeleka
huduma kwenye maeneo yenye changamoto za Maji,Elimu Afya na miundombinu.
‘’Sisi
tunapaswa kuwa katikati kuwasemea wasiokuwa na sauti ili waheshimiwa wasikie
waweze kukaa na kupanga Bajeti ii wanachi wenye uhitaji na huduma hizo wapatiwe
huduma’’
Katika
maadhimisho hayo ya Uhuru wa vyombo vya Habari waandishi wa Habari katika mkoa
wa Katavi wamepata fursa ya kupatiwa elimu kuhusu habari zinazo husu Masuala ya
kipolisi yaliyotolewa na maafisa kutoka jeshi la polisi mkoa wa katavi pamoja
na Elimu kuhusu Madhara ya Rushwa yaliyotolewa na maafisa kutoka Taasisi ya
kuzuia na kupambana na Rushwa Takukuru mkoa wa katavi.
Maadhimisho ya uhuru wa Vyombo vya habari kwa mwaka 2023 yamebebwa na kaulimbiu inayosema kuunda Mstakabali wa haki uhuru wa kujieleza kamakichocheo cha haki nyingine zote za Kibinadamu.