Madiwani katika halmashauri ya Nsimbo mkoa wa katavi wakiwa katika kikao cha Balaza la Madiwani |
Baraza la Madiwani katika Halmashauri yaNsimbo mkoa wa Katavi wameiomba serikali kupitia wizara ya Mali
asili na utalii kuja na Mpango maalumu wa kuwavuna wanyama aina ya Mamba kwenye
Mto Ugalla kwani wamekuwa wakisabisha vifo kwa wananchi na wanafunzi wanapo
kwenda kuteka maji kwenye mto huo.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Nsimbo katikati Charles Halawa pamoja na mkurugenzi wa halmashauri ya Nsimbo Mohamed Ramadhan wa Kwanza kulia na Adam Chalamila Makamu mwenyekiti kwenye kikao hicho |
Balaza la Madiwani katika halmashauri yaNsimbo mkoa wa Katavi wameiomba serikali kupitia wizara ya Mali asili na utalii kuja na Mpango maalumu wa kuwavuna wanyama aina ya Mamba kwenye Mto Ugalla kwani wamekuwa wakisabisha vifo kwa wananchi na wanafunzi wanapo kwenda kuteka maji kwenye mto huo.
Elieza Fyula Diwani wa kata ya
Mtapenda amiibua hoja hiyo wakati akichangia hoja za kamati kwenye baraza hilo
amesema katika kipindi cha nyuma waliomba ushauri huo wa kuwavuna Mamba hao
kwenye Mto Ugalla.
Fyula anasema ‘’huko nyuma
Mamba waliua watu wengi sana Ugalla na tulishauri ipelekwe kampuni na kupewa
zabuni kwaajili ya kuwinda wale wanyama wakapungua na maisha ya watu
yakasalimika sasa hii hali imejirudia labda Mamba wamezaana sana’’
Amesema nivyema hatua zikachukuliwa
haraka ili maiasha ya wananchi yaendelee kama kawaida.
Baadhi ya Madiwani katika Halmashauri ya Nsimbo mkoa wa Katavi wakiwa katika kikao cha Baraza la Madiwani |
Kasanga ‘’anasema Chanzo cha
kuliwa wananchi na Mamba nipamoja na uhaba wa Maji wanaenda kufata maji kwenye
sehemu ambayo Mamba wapo na mamba wanakaa pale kwa kuwasubili ‘’
Amesema tayari Serikali imeleta
fedha kwaajili ya ujenzi wa Mradi wa Maji ambapo zaidi ya shilingi milioni 700
zimeletwa hatua ambayo itapunguza tatizo hilo pindi utakapo kamilika kwa
wananchi wa maeneo ya katambike ambao wameonekana kuwa wahanga wa kutafunwa na
Mamba hao.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya
Nsimbo Charles Halawa ambae pia ni Diwani wa Kata ya Ugalla amesema tatizo hilo
kwenye Kata ya ugalla lipo na hatua lazima zichuliwe
‘’Hao wanachi wanaozungumnzwa
wapo kwenye Kata yangu juzi tumempoteza Mtoto aitwae Mrisho Msombola mwenye
miaka 14 alikuwa mwanafunzi wa Darasa la Saba ameondoka na mamba kwahiyo
lipozungumziwa suala la Mamba tuwesiliazi kidogo’’ amesema Halawa
‘’tulifanya jukumu la kuandika
Barua wizara ya mali asili kwaajili ya kuomba sasa kibali cha kununwa na mpaka
sasa bado hatujapokea majibu yeyote ya kukubaliwa kibali hicho au la ‘’amesema
Ramadhani
Jonas Mathas Afisa afisa mali asili Halmashauri ya Nsimbo amesema tayari wameanza kuchukua hatua kwa kuweka alama ambazo Mamba hao wameonekana wakionekana mara kwa mara