KATAVI HIPPOS HALF MARATHON


Joseph Katembo-Mratibu Kamati ya ufundi Katavi Hippos Half Marathon (kushoto), Beltila Kaphipa Mkurugenzi wa Mama Afrika Tz Vision Sports na Waandaaji wa Katavi Hippos Half Marathon (katikati) na Rhoda Michael-Afisa Utalii Bodi ya Utalii Tanzania (kulia) 

Na Mwandishi wetu,Katavi

Wakazi wa Mkoa wa Katavi wameaswa kujitokeza kwa wingi kushiriki katika Mbio za Katavi Hippos Half Marathon zilizoandaliwa na Taasisi ya Mama Afrika Tanzania Vision Sports kwa ajili ya kutangaza vivutio vilivyopo ndani ya Mkoa wa Katavi.

Akizungumza na Waandishi wa habari kuelekea Mbio hizo zitakazo fanyika July 16,2022 Mkurugenzi wa Mama Afrika na Muandaaji wa Katavi Hippos Half Marathon Beltila Kaphipa amesema  wameandaa Mbio hizo kwa lengo la kukuza Utalii wa Mkoa wa Katavi na kuvitangaza vivutio vilivyopo ndani ya Mkoa.

"Mbio hizi tumezipa jina la Katavi Hippos Half Marathon kwa sababu Katavi ni Hifadhi ya Taifa yenye viboko wengi na wakubwa ambao hawapatikani katika Hifadhi yoyote hapa nchini,kwa hiyo tukaona ni vyema tujivunie Utalii uliopo katika Mkoa wetu wa Katavi kupitia Hifadhi yetu ya Katavi"alifafanua Kaphipa

Kuhusu zawadi kwa washindi mbalimbali katika Mbio hizo amesema washindi wataibuka na vitita vya fedha pamoja na medali ambapo washindi watatu kwa jinsia zote mbili wakike na wakiume watakao kimbia kilomita 10 na kilomita 21.1 watapatiwa zawadi.

Beltila Kaphipa Mkurugenzi wa Mama Afrika Tanzania Vision Sports na Waandaaji wa Katavi Hippos Half Marathon Mkoa wa Katavi,July 16,2022

Mshindi wa kwanza atazawadia shilingi laki tatu, mshindi wa pili shilingi laki mbili na mshindi wa tatu shilingi laki moja.

Kwa upande wao Bodi ya Utalii Tanzania kupitia kwa Mwakilishi wao Afisa Utalii Rhoda Michael  amesema Bodi hiyo wanaunga mkono Wadau mbalimbali Kama Taasisi ya Mama Afrika ili kukuza Utalii wa Tanzania.

Nao Wananchi wa Mkoa wa Katavi akiwepo Godwin Msemo amesema wapo tayari kushiriki Mbio hizo za Katavi Hippos Marathon zenye lengo la kuutangaza Mkoa wa Katavi na vivutio yake vilivyopo.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages