ZIARA YA MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DK.PHILLIP MPANGO MKOA WA KATAVI

 

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko akitoa Taarifa ya ujio wa Makamu  wa Rais Mkoa wa Katavi kuanzia July 21 Hadi 25,2022 Dk Phillip Isdory Mpango kutembelea miradi ya Maendeleo ndani ya Mkoa huo.


Na Mwandishi wetu,Katavi.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Philip Mpango,anatarajiwa kufanya ziara ya siku tano mkoani Katavi, kwa lengo la kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa  na kuzungumza na wakazi wa Mkoa huo.

Akitoa taarifa ya ujio wake kwa waandishi wa habari Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko, amesema Dk Mpango atafanya ziara Julai 21 hadi 25 mwaka huu ambapo moja ya miradi atakayoitembelea ni pamoja na kituo cha kupozea umeme wa gridi ya Taifa kutokea Sikonge Mkoani Tabora kuja Mkoa wa Katavi.

Amesema mbali na mradi huo pia ataweka jiwe la msingi kituo cha afya kibaoni Halmashauri ya Mpimbwe nakuzindua jengo la Halmashauri hiyo pamoja na kuzungumza na wananchi wa Halmashauri hiyo.

Mrindoko amesema Julai 23 Mpango atafanya ziara katika Wilaya ya Tanganyika kijiji cha Katuma ambapo atakabidhi hundi kwa vijiji nane ambavyo vina husika na utunzaji wa mazingira na kuelekea katika kijiji cha Sibwesa ambapo atazindua mradi wa maji nakuzungumza na wananchi.

Aidha Mrindoko amesema kuna tatizo la kukatika kwa umeme mara kwa mara na  kubainisha sababu zinazopelekea kukatika kwa umeme huo ni ongezeko la  matumizi ya umeme kutokana na wingi wa watu wanaotumia umeme huo.

"Kama mnavyofahamu Mkoa wetu unapokea umeme unaozalishwa kwa mafuta na mashine za jenereta na umeme unaozalishwa kwasasa hivi ni megawati tano kutokana na kuongezeka kwa matumizi zinahitajika megawati sita.

Aliendelea kubainisha kuwa Serikali haijakaa kimya kwani swala hilo inaendelea kulifuatilia kwa kushirikiana na Waziri wa Nishati na kwasasa hivi kuna suluhisho la muda mrefu ambalo ni kuleta umeme wa gridi ya Taifa kutoka Mkoa wa Tabora na mradi huo umeishaanza na unatarajia kukamilika Disemba 2023.

Mrindoko amesema utatuzi wa hivi karibuni tayari Wizara imeishapata mashine Mkoani Arusha na itahamishwa kuletwa Mkoa wa Katavi kwaajili ya kuongeza nguvu mashine zilizopo kwa sasa.

Hatahivyo Mrindoko amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika mapokezi ya Makamu huyo ilikufanikisha kwa ziara hiyo kwenda vizuri.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages