ABAKWA NA KIKONGWE WA MIAKA 62 KUSAFISHIWA NYOTA YA BIASHARA


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi ACP Ali Makame Hamad akitoa taarifa   ya kukamatwa kwa Mganga wa kienyeji  Simbuka  Makande(62)  mkazi wa  kijiji cha  Magengase  Mkoa wa Tabora  anayetuhumiwa kumbaka Mfanyabiashara wa madini ya dhahabu(32) jina limehifadhiwa mkazi wa Kijiji cha Katuma  Wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi baada ya kumrubuni kuwa atamsafishia nyota(Picha na Walter MguIuchuma)


Na Walter MguIuchuma,Katavi .


Jeshi la  Polisi  Mkoa wa Katavi linamshikilia Mzee mmoja aliyefahamika kwa jina la  Simbuka  Makande (62) Mganga wa kienyeji  mkazi wa Kijiji cha  Magengase  Mkoa wa Tabora  kwa tuhuma za kumbaka  mwanamke (32) Mfanyabiashara wa madini ya dhahabu Mkazi wa Kijiji cha Katuma Wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi baada ya  kumrubuni kuwa atamsafishia nyota ya kupata mali.

 

 Kamanda wa Polisi wa Mkoa  wa  Katavi  ACP Ali Makame  Hamad  amewaambia Waandishi wa Habari kuwa  Mganga huyo wa Kienyeji  alikuwa ametokea Mkoani Tabora na kufikia katika Kijiji hicho cha Katuma na kukodi chumba kwenye nyumba ya kulala wageni inayoitwa  Bunga .

 

Ambapo mhanga wa tukio hilo nae alikuwa amefikia kwenye nyumba hiyo ya kulala wageni   huku akiwa anaendelea kufanya biashara  yake ya madini ya dhahabu yanayochimbwa kwenye  Kijiji hicho cha Katuma .

 

Kamanda Makame  aliendelea kueleza kuwa ndipo mwanamke huyo alipokutana na Mganga Makande na alimweleza  mwanamke huyo kuwa anao uwezo wa  kuwasafishia watu nyota zao  ili waweze kupata mafanikio kwenye shughuli zao na moja ya masharti yake ni kufanya nae mapenzi .

 

Alisema ndipo Mganga huyo  alimrubuni  mhanga  na kufanya nae mapenzi kwa nyakati tofauti tofauti  na pia mhanga aliweza kumpatia mganga   kiasi cha shilingi  milioni moja na elfu sitini .

 

Amebainisha kuwa  Mganga  huyo pia anatuhumiwa kufanya vitendo hivyo  kwa watu watatu Mkoani Katavi na kujichukulia kwa watu hao kiasi cha shilingi milioni  nne na laki sita.

 

Amekuwa  pia akiwatapeli watu hao kuwa amesha wasaidia viongozi wengi  kupata mafanikio  na kisha kufanya nao mapenzi  kwa kuwarubuni  kuwa atawasaidia kupata mafanikio  kama hayo  katika biashara  zao na maisha kwa ujumla .

 

Kamanda Makame amesema mtuhumiwa  amekamatwa na enaendelea kuhojiwa na Jeshi la Polisi  na mara upelelezi  utakapo kamilika  atafikishwa Mahakamani  kujibu tuhuma zinazomkabili.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages