MKOA WA KATAVI UMEFANIKIWA KUYAFIKIA MAENEO YOTE WATU WALIOTAKIWA KUHESABIWA .


Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko akiwa katika  Mtaa wa Mpanda Hoteli Manispaa ya Mpanda nyumbani kwa Mzee Alkado Mwima akikagua maendeleo ya zoezi la sensa linaloendelea ikiwa ni siku ya kwanza ya zoezi hilo(Picha na Walter MguIuchuma)


Na  Walter Mguluchuma

   Katavi .


 Mkoa wa Katavi umefanikiwa kuyafikia maeneo yote ya muhimi kwa wakati ambayo watu walitakiwa kuhesabiwa kuanzia saa sita na dakika moja usiku yakiwepo maeneo ya  stendi zote zate nyumba za kulala wageni ,bar.

Hospitalini .magereza. Watoto wa mitaani  na kwenye treni ya abiria inayofanya safiri ya kutoka Mpanda kwenda Tabora .

 

 Pia kwenye zoezi hilo la Sensa ya watu na Makazi linaloendelea kufanyika Mkoani  Katavi hadi sasa hakuna changamoto ypyote ambayo imeisha jitokeza  na wananchi wamehamasika  sana na wanatowa ushirikiano mkubwa kwa makarani wa sensa .

 

 Akizungumza na wandishi wa Habari mbele  ya wananchi wa Mkoa wa Katavi   Mwanavua Mrindoko kwenye maeneo mbalimbali aliyokuwa akiyatembelea katika Manispaa ya Mpanda wakati akikagua maendeleo ya  zoezi la sensa alisema kuwamaeneo yote ya muhimu  yameweza kufikiwa kwenye zoezi la sensa kwa wakati  na na bila kuwepo kwa changamoto yoyote ile hadi sasa.

 

Amebainisha kuwa wananchi wa Mkoa wa Katavi wamehasika sana kwenye zoezi hili na wako tayari kuhesabiwa      ambapo kwenye zoezi hili wananchi wamekuwa wakitowa ushirikiano mkubwa sana huku hali  ikiwa  ya maeneo yote ni salama .

 

 Mrindoko alisema kuwa  kwenye zoezi hilo wanahakikisha linafanikiwa kwa asilimia   mia moja na watu wote wanafikiwa na kuhesabiwa  kama ilivyokusudiwa  bila kujali hali ya jografia ilivyo ya Mkoa huu.

 

 Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi  Haasan Abasi Rugwa  amesema kuwa zoezi hili katika Mkoa wa Katavi limeanza kwa ufanisi mkubwa huku ulinzi na usalama ukiwa umeimalika  na mpaka sasa hakuna malalamiko yoyote ya kutoka kwa wananchi kutokana  kazi kubwa ambayo imefanywa ya zoezi la sensa kwenye Mkoa wa Katavi .

 

 Hivyo amewataka kila wananchi wa Mkoa wa  Katavi kuhakikisha anahesabiwa na ndio mkakati ambao Mkoa umejiwakea wa kuhakikisha  hakuna mtu hata mmoja ambae hata hesabiwa kwenye zoezi hili .

 

 Karani wa Senza wa eneo namba  002  huko katika eneo la Ilembo  A siton Kajiba  amesema kuwa zoezi hilo kwa upande wake limekuwa likienda vizuri kutokana na ushirikiano  kutoka kwa wana wananchi kwani kila Kaya ambayo amekuwa akiifikia amekuwa amekuta wakiwa  tayari wameandaa nyaraka muhimu zinazo hitajika kwenye zoezi hilo hali ambayo inaonyesha kuwa watu wamekuwa na uwelewa  wa umuhimu wa sensa ya watu na makazi.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages