MANISPAA YA MPANDA YAVUKA LENGO LA MAKUSANYO YA NDANI 2021/2022


Kikao Cha Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Mpanda katika Ukumbi wa Manispaa Mkoa wa Katavi.

 Na Walter MguIuchuma,Mpanda.


 HALMASHAURI ya Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi imefanikiwa kuvuka lengo la  fedha  za  makusanyo ya ndani kwa  mwaka wa fedha wa 2021/2022 kwa zaidi ya asilimia 100 kutokana na usimamizi  mzuri wa kukusanya mapato .


 Hayo yameelezwa na Afisa  mapato wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Elias Samoja wakati alipokuwa akitoa taarifa ya makusanyo ya  fedha za ndani kwa mwaka wa fedha uliopita  kwenye kikao cha  Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Mpanda kilichofanyika kwenye ukumbi wa Manispaa hiyo.

 

 Alisema kuwa kwa mwaka wa fedha uliopita Manispaa ya Mpanda waliweka lengo la kukusanya mapato ya ndani kiasi cha shilingi Bilioni  2.9 hata hivyo wameweza kufanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi Bilioni 3.2 ikiwa ni sawa na asilimia 104.

 

Samoja amebainisha kuwa mafanikio hayo yametokana na usimamizi mzuri wa ukusanyaji wa mapato waliouweka kwenye Manispaa hiyo pamoja na ushirikiano mkubwa uliopo wa ukusanyaji wa mapato   baina ya Madiwani na Watumishi wa Halmashauri .

 

 Afisa Mipango wa  Manispaa ya Mpanda  Waza Kiusasi alieleza kuwa  kati ya fedha hizo za makusanyo ya ndani  asimila 49 wamepeleka kwenye miradi mbali mbali  ya maendeleo  inayotekelezwa  kwa ajili ya kuwapatia wananchi huduma kama za Afya , Elimu, maji na mikopo kwa makundi maalumu .

 

Meya wa Manispaa ya Mpanda  Haidary Sumry  alieleza kuwa lengo la  kufanyika kwa mkutano mkuu wa mwaka wa baraza la  Madiwani wa Manispaa hiyo  ni kujadili  mafaniko  na changamoto    katika mwaka wa fedha uliopita .

 

Hivyo aliwaomba Madiwani na watumishi wa Halmashauri hiyo kuendelea kushirikiana  zaidi ili kuhakikisha mapato yao ya ndani hayapotei hata kidogo  na yazidi kuongezeka na kufanya  huduma ziendelee kuwa bora zaidi kwa wakazi wa Manispaa hiyo ya Mpanda.

 

Diwani wa Kata ya Majengo William Mbogo aliongeza kuwa kuongezeka kwa ukusanyaji wa mapato na kuwa mengi zaidi kumeweza kufanya miradi mbambali kuongezeka kwenye Kata zote za Halmashauri hiyo .

Diwani wa kata ya Majengo William Mboga akichangia katika kikao Cha Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi na kuipongeza Serikali kwa kuleta miradi mingi ya Maendeleo kwa wakati mmoja tofauti na ilivyokuwa kipindi cha nyuma.(Picha na Walter MguIuchuma)


Alisema yeye amedumu kwenye Udiwani kwa kipindi cha sita sasa  zamani alikuwa akipata mradi wa kujengewa hata darasa moja alikuwa anajisifu lakini kwa sasa miradi kupelekwa kwa wingi imekuwa ni jambo la kawaida kwenye kila kata .

 

Nae Diwani wa   Kata ya Mwamkulu Kalipi Katani aliliomba Baraza hilo  liangalie utaratibu wa kutunga sheria ndogo itakayowataka kila mzazi mwenye mtoto

kuchangia chakula shuleni kwa kila mwanafunzi anae soma Shule ya  msingi  hadi Sekondari

 

Alieleza kuwa  kwa sasa   sheria hiyo ndogo haipo kwenye Halmashauri hiyo hivyo inawafanya wazazi walio wengi watoto wao  wanashida na njaa kwenye Shule kutokana na kutokuwepo kwa  chakula shuleni.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages