WATUMISHI KATAVI WAIPA HEKO SERIKALI NYONGEZA YA MSHAHARA

 

Mwalimu Fespenda Matembo wa shule ya msingi Msakila Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi akizungumza leo mapema na vyombo vya habari.

Na Walter Mguluchuma KTPC,Katavi.

Baadhi ya watumishi wa Idara   mbalimbali zilipo katika Mkoa wa Katavi  wameishukuru Serikali kwa kuwaongezea  mishahara   na kuwapandisha madaraja kwani  walikuwa wakiishi kwa muda wa zaidi ya miaka sita kwa matumaini wakisubulia nyongeza na kupandishwa madaraja.

Baadhi ya watumishi hao Fespenda Matembo,Mwalimu wa shule ya Msingi Msakila Manispaa ya Mpanda alieleza kuwa yeye kama mwalimu na walimu wenzake walikuwa wakiishi kwa matumiani  kwa zaidi ya miaka sita wakisubilia nyongeza ya mshahara.

Lakini rais  Samia Suluhu Hassain wakati wa sherehe za Mei Mosi mwaka huu zilizofanyika Mkoa wa Dodoma aliahidi kuongeza mshahara kwa watumishi kwa asilimia 23 na kweli ametekeleza ahadi hiyo hali ambayo inachochea kufanya kazi kwa utulivu zaidi.

Mwl Fespenda amebainisha kuwa kiasi kilichoongezwa sio haba hata kidogo kwani kimewanufaisha watumishi kulingana na ngazi zao za mishahara kuanzia mishahara ya ngazi ya chini hadi ngazi ya juu.

 

Bonipanye Nkolonko,Mtumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi  alimshukuru rais kwa nyongeza hiyo ya mshahara na anaimani kuwa kwa kuanza kuongeza misharaha upo uwezekano wa kuongeza kila mwaka.

Alisema wapo baadhi ya watu ambao hata wakipewa kidogo huwa hawashukuru na hata wakipewa kikubwa vilevile huwa hawashukuru kwani nyongeza iliyotolewa inawasaidia watumishi kwani wapo walioongezewa hadi Tsh 70,000/-.



Mwalimu Abel Mpepo wa shule ya msingi Kashato anaishukuru serikali kwa  kumuongezea kiasi cha Tsh 30,000/- na pia amepunguziwa mzingo aliokuwa nao wa matibabu ya kuongezewa muda wa watoto wategemezi wake kutoka miaka 18 hadi miaka 22 wakati hapo awali mwisho wa wategeemezi wote waliokuwa wanatibiwa na bima ya afya mwisho miaka 18.

 

Mwl Abeli alieleza kuwa mbali ya nyongeza ya mshahara wanaipongeza serikali kwa kufutiwa faini ya malipo kutoka bodi ya mikopo ambapo yeye binafsi alikuwa anadaiwa milioni 14 ikiwa amefutiwa mil 4  hali ambapo imemfanya mwenzi huu kuchukua mshahara jinsi ulivyo.

 

Schorastica Mathias ambaye ni mwalimu wa sekondari Kasimba Manispaa ya Mpanda amewaomba Watanzania waendelee kumwombea rais Samia Suluhu Hassain aendelee kuwa na afya njema ili azidi kuwatumikia Watazania.

 

Mwl Schorastica alieleza kuwa rais amefanya jambo kubwa la kuwaongezea mishahara ya kuwapandisha madaraja kwani inaonesha namna ambavyo anavyowajali watumishi na Watanzania kwa ujumla kwani ameweza pia kufuta ada ya shule za ngazi ya kidato cha tano na sita.

 

 


 

 

 

 

 

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages