MBUNGE AOMBA SULUHU YA MIGOGORO YA ARDHI BAINA YA WAFUGAJI NA WAKULIMA SERIKALI

Mbunge wa Jimbo la Mpanda Vijijini Mkoa wa Katavi Moshi Seleman Kakoso akiwahutubia wakazi wa Jimbo hilo katika uwanja wa shule ya Msingi Majalila kwenye Mkutano wa hadhara.


Na  Walter Mguluchuma

   Katavi .

Mbunge wa Jimbo la Mpanda Vijijini katika Wilaya ya Tanganyika Moshi  Selemani Kakoso ameiomba  Serikali ya Wilaya ya Tanganyika  kuwashirikisha wadau mbambali watakaosaidia kuondoa kero ya migogoro ya ardhi baina ya Wakulima na Wafugaji  ili waweze kuishi kwa amani kwani imekuwa kero kubwa kwa Wilaya hiyo.


Ombi hilo amelitoka  jana wakati akiwahutubia mamia ya wakazi wa Kata ya Ntongwe kwenye  mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Shule ya Msingi Majalila  Wilayani Tanganyika.


Kakoso amebainisha kuwa kupitia mikutano ya hadhara kwenye Kata 16 na vijiji 55 alivyotembelea  katika ziara yake Jimboni humo iliyochukua zaidi ya mwezi mmoja swala la migogoro kwa wakulima  na wafugaji limekuwa kero kubwa iliyokuwa ikiibuliwa na wananchi karibu kila Kijiji alichofanya mikutano katika Wilaya hiyo ya Tanganyika .

 

Alisema  migogoro hiyo imekuwa ikichangiwa na mambo mbali mbali  ikiwemo wananchi wenyewe kuwauzia wafugaji maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya kilimo na sio kulishia mifugo.


Sambamba na Viongozi wa Vijiji na Vitongoji  kuwauzia wafugaji maeneo ya ardhi ambayo hayastahili kulishia mifugo na kuwachanganya pamoja na Wakulima hivyo kusababisha migogoro baina yao.


"….kwa bahati mbaya  wafugaji hawathamini mazao ya wakulima wanayokuwa wameyalima hivyo basi  ninachokiona mimi Mbunge  kuna hatari kubwa inayokuja ya mgogoro mkubwa sana  kwenye Wilaya ya Tanganyika baina ya wakulima na wafugaji endapo hatua za haraka sana hazitachukuliwa"alifafanua Kakoso

 

Aidha amesema kuwa  kumekuwepo na tatizo  la Halmashauri ya Tanganyika kuweka  bikoni  za mipaka ya Hifadhi hadi kwenye maeneo ya wakulima jambo ambalo sio sahihi kabisa .

 

Amemwomba Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika  Onesmo Buswelu  na Kamati yake ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya washirikishe na wadau wengine ili waweze kutafuta suluhu ya kuwapatanisha wafugaji na wakulima waweze kuishi kwa amani .

 

Nae  Tausi  Mrisho mkazi wa Kijiji cha Majalila alisema kuwa hali sio nzuri baina yao na wafugaji kwani wafugaji wamekuwa na tabia  ya kulishia mifugo yao kwa wakulima na yeye binafsi kwenye msimu huu nusu ekari nzima ya mpunga wake imeliwa na mifugo na kila wanapokuwa wakiwauliza wafugaji kwani  mifugo yao wanaipeleka kwenye mashamba yao wamekuwa wakiwashambulia kwa vitisho vya kuwapiga .

 

Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Onesmo Busweru alieleza kuwa kero hiyo iliyotolewa na Mbunge ya  mgogoro wa wakulima na wafugaji ni sauti ya wananchi hivyo swala hilo watalifanyia kazi mapema.

 

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages