WATUMISHI WA HALMASHAURI YA TANGANYIKA WAKO HATARINI KUONDOKA KWENYE VITUO VYAO VYA KAZI .

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Tanganyika Yassin Kiberiti

Na Walter Mguluchuma,Tanganyika


Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika Mkoani Katavi  na wale wa Serikali Kuu wanaofanya kazi kwenye  Makazi ya wakimbizi eneo la Mishamo wako hatarini kuondoka kwenye vituo vyao vya kazi kutokana na kero wanayoipata ya kudaiwa vibali  na Mkuu wa Makazi hayo ya Wakimbizi pindi wanapohitaji kutoka kwenye eneo hilo .
 
Kero hiyo ya Watumishi wanaofanya kazi katika Makazi ya Wakimbizi Mishamo imetolewa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Tanganyika Yassin Kiberiti wakati wa mkutano wa hadhara uliondaliwa na Mbuge wa Jimbo la Mpanda Vijijini Moshi Kakoso uliofanyika katika  Uwanja wa michezo wa shule ya Msingi Majalila .


Wakazi wa Jimbo la Mpanda Vijijini Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika wakiwa katika Mkutano wa hadhara  wa Mbunge wa Jimbo hilo Moshi Kakoso katika Uwanja wa Shule ya Msingi Majalila

Amebainisha kuwa eneo hilo la makazi ya wakimbizi Mishamo  mbali ya kuishi watumishi hao pia wanaishi wazawa na waliokuwa Raia wa Nchi ya Burundi ambao Serikali imesha wapatia uraia wa Tanzania na baadhi ya raia wachache sana wa Nchi ya Burundi .
 
Kibiriti amesema kuwa Watumishi hao wamekuwa wakipata kero pindi wanapotaka kutoka kwenye eneo hilo la kambi kwenda kujipatia mahitaji na huduma ambazo hazipo katika maeneo hayo na kutakiwa kutoka kwa vibali vya Mkuu wa Makazi .

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages