MCHEPUKO WA BI MDOGO ANUSURIKA KIFO

 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi ACP Ali Makame Hamad akitoa taarifa ya matukio mbalimbali yaliyojitokeza Katika Mkoa wa Katavi mbele ya Waandishi wa habari(Picha na Walter MguIuchuma)

Na Walter MguIuchuma,Katavi.

 

 Mtu mmoja aliyefahamika   kwa jina la  Machia  Mbasa (General)miaka  65 Mkazi wa Kijiji cha Lwafe  Wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kupanga njama za kumuua  Mabula Ntemange(37) kwa kumtuhumu  kuwa na mahusiano ya kimapenzi  na  mke wake mdogo  wakati  yeye alipokuwa gerezani .


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi Ally Hamad Makame amethibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo na Jeshi la Polisi kufutia taarifa zilizowafikia za mtuhumiwa  kutekeleza mauaji hayo yaliyosababishwa na wivu wa kimapenzi .


Kamanda Makame alisema pia mtuhumiwa alikuwa akimtuhumu Mabula Ntemange kuchukua kodi kwenye vibanda vyake ya biashara  alivyovijenga eneo hilo la Lwafe na kwenda  kustarehe na mke wake huyo mdogo wakati yeye akiwa kwenye gereza la mahabusu Mpanda Mjini kwa tuhuma za mauaji.


"...baada ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi  kupata taarifa hizo walichukua hatua za haraka na kufanikiwa kuzuia jaribio hilo la mauaji kwa kumkamata mtuhumiwa Mbasa kabla haja tekeleza mauaji hayo"alibainisha Kamanda Makame.


Hivyo mtuhumiwa amekamatwa na kufikishwa kituo cha Polisi kwa ajili ya mahojiano zaidi juu ya kutaka kutekeleza kitendo hicho cha kukatisha uhai wa binadamu mwenzake ambapo kisheria ni kosa kuuwa kwani kila mtu anahaki ya kuishi.

 

Baada ya kuhojiwa mtuhumiwa  alikiri  kupanga njama  za kutaka kufanya hivyo kutokana na hasira ya jirani yake huyo kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mke wake mdogo anayempenda wakati yeye akiwa anasota mahabusu.

 

Kamanda Makame amebaisha kuwa mtuhumiwa  huyo alikuwa amewakodi  wauaji wawili  kutoka Kaliua  Mkoani Tabora  na baada  ya wauaji hao  kufika Mjini Mpanda walipokelewa  na mtuhumiwa na kisha  walihifadhiwa  kwa ajili ya kusubiri  kutekeleza mauaji hayo.


Mbali  ya kupanga mauaji hayo mtuhumia  Machia  Mbasa amekuwa pia  akituma ujumbe wa vitisho  vya mauaji  kwa watu wawili  ambao ni Charles Lugembe  na  Dogani  Malima wote wakazi wa Kijiji cha Mwamkulu Manispaa ya Mpanda .

 

Mtuhumiwa  bado anaendelea kuhojiwa na Jeshi la Polisi ili kubaini  mtandao  mzima anaoshirikiana nao kutekeleza  vitendo vya mauaji  na mara baada ya upelelezi kukamilika atafikishwa Mahakamani kujibu tuhuma zinazo mkabili.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages