MWIZI WA PIKIPIKI KWA KUTUMIA FUNGUO BANDIA KORTINI KATAVI

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi ACP Ally Hamad Makame akionyesha mbele ya Waandishi wa Habari pikipiki tano alizokamatwa nazo mtuhumiwa maarufu wa wizi wa pikipiki ambazo alikuwa ameziiba kwenye maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Katav(Picha na Walter Mguluchuma)


Na Walter MguIuchuma,
Katavi


Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi limefanikiwa kumkamata mtuhumiwa maarufu wa wizi wa pikipiki anaefahamika kwa jina la Laurenti Lazaro (61) Mkazi wa  Kanoge Wilaya ya Mpanda akiwa  ameiba  pikipiki tano za watu tofauti tofauti.


Kamanda wa Polisi  Mkoa wa Katavi Ally Hamad Makame amewaambia Waandishi wa Habari ofisini kwake mtuhumiwa huyo alikamatwa hapo juzi majira ya saa kumi jioni  huko katika Mtaa wa Msufini Kata ya  Uwanja wa Ndege Manispaa ya Mpanda.


Kabla ya kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi  waliandaa msako mkali  wa kupambana na uhalifu  na waliweza kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo  akiwa na pikipiki ya wizi yenye Namba za usajiri   MC  915 CDV   aina ya  HONLG yenye rangi nyekundu.


Kamanda  Ally Makame alisema  baada ya mtuhumiwa huyo kukamatwa  na kufanyiwa mahojiano  ya kina  alikiri kuwa aliiba pikipiki  nyingine nne  kwenye maeneo tofauti tofauti ya Mkoa wa Katavi  na aliweza kwenda kuzionyesha pikipiki hizo.


Ambapo  katika msako huo  walifanikiwa  kupata pikipiki hizo nne na  kufanya jumla ya pikipiki tano alizokuwa ameiba mtuhumiwa huyo  zenye Namba za usajiri  MC,445 AAA ina  ya SANLG rangi nyekundu , MC  553 ADM  aina ya SANLG rangi nyekundu,MC 468 CUC aina ya  SINOREY  na MC  802 CQJ aina ya  SYNOTEY.


Makame alieleza kuwa mtuhumiwa  huyo alikuwa akiiba kwa kutumia mbinu ya kutembea na funguo  bandia ambazo  ndizo alikuwa  akizitumia  kuibia pikipiki zinazokuwa zimepakiwa  kwenye maeneo mbalimbali  na wamiliki wa pikipiki hizo.


Mtuhumiwa bado anaendelea  kuhojiwa  ili kuweza kuwapata washiriki  wake wanao shirikiana nae  katika kufanya wizi huo   wa pikipiki na  mara baada ya upelelezi kukamilika mshitakiwa atafikishwa mahakamani  kujibu tuhuma zinazo mkabili.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages