KIONGOZI MWENGE WA UHURU WALIMU WANASUSIWA USIMAMIZI WA UJENZI WA MIRADI MASHULENI.

 

Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa mwaka 2022,Sahili Nyanzabara Geraruma (kulia) akihutubia wananchi walio hudhuria kwenye mbio za mwenge katika halmashauri ya Nsimbo Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi.-(Picha na Paul Mathias)

Na George Mwigulu,Nsimbo.

Kiongozi wa mbio Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2022,Sahili Nyanzabara Geraruma ametoa wito kwa wakurugenzi wa wataalamu wao kutokuwasusia walimu mashuleni juu ya usimamizi wa ujenzi wa miradi ya maendeleo badala yake watumie taaluma zao kusimamia miradi hiyo.

Mkuu wa wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi,Jamila Yusuph akipokea Mwenge wa Uhuru katika viwanja vya shule ya msingi Uruwira Halmashauri ya Nsimbo- (Picha na Paul Mathias).

Kiongozi wa mbio Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2022,Sahili Nyanzabara Geraruma ametoa wito kwa wakurugenzi wa wataalamu wao kutokuwasusia walimu mashuleni juu ya usimamizi wa ujenzi wa miradi ya maendeleo badala yake watumie taaluma zao kusimamia miradi hiyo.

Kauli hiyo ameitowa wakati akizindua vyumba vinne vya madarasa katika shule ya sekondari Uruwira,Halmashauri ya Nsimbo Mkoa wa Katavi ambapo alieleza kuwa hali ya watumishi kubaki maofisini ni kikwazo cha kufanikisha ubora wa ujezi miradi hiyo.

Geraruma amesema licha ya watumishi kufahamu kuwa ujezi wa miradi inatekelezwa na halmashauri chini ya wakurugenzi na wataalamu wake lakini taaluma zao wameshindwa kuzifanyia kazi.

Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa mwaka 2022,Sahili Nyanzabata Geraruma akikangua madarasa katika shule ya sekondari Uruwira halmashauri ya Nsimbo yaliyojengwa kwa fedha za UVIKO-19- (Picha na Paul Mathias)

Amebainisha kuwa vocha zinaadaliwa na hakuna madokezo wala hakuna nyaraka muhimu lakini watu wanalipwa fedha,Kitendo ambacho kinaashiria kuwepo kwa ubadhirifu wa fedha za serikali.

Kiongozi huyo ya mbio za Mwege wa Uhuru alisikitika kuona fedha kupelekwa kwenye mashule na kazi ya usimamizi wa ujenzi wa miradi kususiwa walimu ambao hawana taaluma hiyo.

"...fedha zinakuja kwenye mashule mnawasusia walimu ambapo huko hakuna wataalamu wa manunuzi,hakuna wahasibu na wala hakuna wahandisi.Kazi mnawaachia walimu alafu nyie mnakaa maofisini" alisema Sahili Nyanzabara Geraruma 

Kutokana na hali hiyo kukithiri nchini,Geraruma alitowa wito kwa watumishi kuanzia ngazi ya wakurugenzi na wataalamu wake kwenda moja kwa moja kusimamia ujenzi wa miradi hiyo ili kuhakikisha inakuwa na ubora kulingana na thamani ya fedha.

Baadhi ya viongozi na wananchi wa halmashauri ya Nsimbo wakisikiliza magizo ya kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa mwaka 2022,Sahili Nyanzabara Geraruma- (Picha na Paul Mathias)

Aidha Kiongozi huyo wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa mwaka 2022 amefanikiwa kutembelea  na kuzindua jumla ya miradi saba ya ujenzi wa miradi ya maendeleo yenye zaidi ya thamani ya milioni 709 katika halmashauri ya Nsimbo.

Baadhi ya miradi iliyozinduliwa ni pamoja na vyumba vinne vya madarasa katika shule ya sekondari Uruwira,kuzindua tmradi wa maji kijiji cha Ikondamoyo,kuzindua wa daraja kijiji cha Ivungwe na Kuzindua mradi wa zahanati kijiji cha Isanjandugu.







Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages